• HABARI MPYA

  Thursday, March 04, 2021

  COASTAL UNION WATIBUA REKODI YA YANGA KUTOFUNGWA, WAICHAPA 2-1 MKWAKWANI, KISINDA AKOSA PENALTI

  Na Mwandishi Wetu, TANGA
  WENYEJI, Coastal Union wamewaangusha vigogo, Yanga SC baada ya kuwachapa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Huo unakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga SC kupoteza msimu huu na kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 22 na kupanda kwa nafasi tano hadi ya 10.
  Pamoja na kufungwa, Yanga SC inayobaki na pointi zake 49 baada ya kucheza mechi 22 sasa, inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi tatu mkononi. 
  Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Raphael Ikambi aliyesaidiwa na Abdallah Rashid na Makame Mdogo, Coastal Union walipata bao lao la kwanza kupitia kwa kijana alyeubuliwa timu ya vijana ya Yanga, Erick Msagati dakika ya 10.
  Msagati alifunga bao hilo dakika moja tu baada ya kiungo Tuisila Kisinda, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuikosesha Yanga bao la mapema baada ya kumpelekea mikononi mkwaju wa penalti kipa wa Coastal Union, Abubakar Abbas Ibrahim kufuatia yeye mwenyewe kuangushwa kwenye boksi.
  Lakini Kisinda, mchezaji huyo wa zamani wa AS Vita ya kwao, Kinshasa akasawazisha makosa yake baada ya kuifunga Yanga SC bao la kusawazisha dakikia ya 39 kwa juhudi binafsi kufuatia kuwazidi maarifa mabeki wa Coastal.
  Chipukizi Mudathir Said akawainua juu Wana Mangush baada ya kuifungia Coastal Union bao la ushindi dakika ya 84 akitumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya Yanga.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Polisi Tanzania imeichapa KMC 1-0 Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Tanzania Prisons imelazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya City Uwanja wa Samora, Sumbawanga mkoani Rukwa na Mtibwa Sugar wametoa sare ya 0-0 na Biashara United Uwanja wa CCM Gairo, Morogoro.
  Kikosi cha Coastal Union kilikuwa; Abubakar Ibrahim, Hassan Kibailo, Hance Masoud, Peter Mwangosi, Paschal Kitenge, Salum Ally, Abdul Suleiman, Francis Mustafa, Sammy Kasikasi/ Mudathir Said dk70, Hamad majimengi na Erick Msagati/ Issa Abushehe dk67.
  Yanga SC; Farouk Shikairo, Kibwana Shomary, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Tonombe Mukoko, Tuisila  Kisinda, Feisal Salum, Michael Sarpong/Yacouba Sogne dk35, Abdul Razak Fiston na Farid Mussa/Deus Kaseke dk50.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION WATIBUA REKODI YA YANGA KUTOFUNGWA, WAICHAPA 2-1 MKWAKWANI, KISINDA AKOSA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top