• HABARI MPYA

  Sunday, March 14, 2021

  BINGWA WA DUNIA WA ZAMANI NDONDI ZA KULIPWA AFARIKI DUNIA


  BINGWA wa ngumi za kulipwa wa dunia wa zamani uzito wa Middle, Marvin Nathaniel Hagler, amefariki dunia jana akiwa ana umri wa miaka 66 – mkewe, Kay G. Hagler amethibitisha.
  Hagler aliyestaafu ndondi 
  baada ya kupigwa kwa utata na Ray Charles ‘Sugar Ray’ Leonard mwaka 1987 akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 62, kati ya hayo 52 akishinda kwa Knockouts, kupigwa matatu na droo mbili kuanzia 1973 hadi 1987.
  Alikuwa bingwa asiyepingika wa uzito wa Middle kuanzia mwaka 1980 kabla ya kupigwa na Leonard ukumbi wa Caesars Palace Jijini Las Vegas Aprili 6, mwaka 1987 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BINGWA WA DUNIA WA ZAMANI NDONDI ZA KULIPWA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top