• HABARI MPYA

  Wednesday, March 31, 2021

  UBELGIJI YAICHAPA BELARUS 8-0 KUFUZU KOMBE LA DUNIA


  LICHA ya kuwapumzisha nyota wake kama Kevin De Bruyne, Romelu Lukaku na Dries Mertens, lakini Ubelgiji jana iliwachapa Belarus 8-0 katika mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia Uwanja wa King Power at Den Dreef, Heverlee.
  Mabao ya Ubelgiji yalifungwa na Michy Batshuayi moja, Hans Vanaken, Leandro Trossard kila mmoja mawili, Jeremy Doku, Denis Praet na Christian Benteke moja kila mmoja.
  Kwa ushindi huo wanafikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi tatu zaidi ya Jamhuri ya Czech inayofuatia, wakati Belarus inabaki na pointi zake tatu sawa na Wales, huku Estonia ambayo haina pointi inashika mkia 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UBELGIJI YAICHAPA BELARUS 8-0 KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top