• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 17, 2021

  NAMUNGO FC YAPIGWA TENA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO, YACHAPWA 2-0 NA PYRAMIDS YA MISRI LEO DAR

  MABAO ya Ramadhani Sobhi dakika ya 71 kwa penalti na Omar Gaber dakika ya 84 leo yameipa Pyramids FC ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Pyramids wanaendelea kuongoza kundi baada ya kukusanya pointi zote sita kwenye mechi mbili za awali, kufuatia kuichapa na Nkana FC ya Zambia 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumatano iliyopita Cairo.
  Namungo yenyewe inaendelea kushika nafasi ya tatu baada ya kufungwa pia na Raja Club Athletic Jijini Casablanca 1-0 Jumatano iliyopita.
  Raja Club Athletic inashika nafasi ya pili kufuatia kukusanya pointi sita pia baada ya leo kuwafunga Nkana FC 2-0 Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAPIGWA TENA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO, YACHAPWA 2-0 NA PYRAMIDS YA MISRI LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top