• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 01, 2020

  LEROY SANE ATUA BAYERN MUNICH KWA DAU LA PAUNI MILIONI 55

  HATMAYE Bayern Munich imefanikisha kumsajili Leroy Sane kwa dau la Pauni Milioni 55 kutoka Manchester City.
  Sane tayari amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ujerumani baada ya kuweka bayana nia yake ya kutaka kuondoka Etihad.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alithaminishwa kwa dau la Pauni Milioni 130 wakati klabu hizo mbili zilipokuwa zinavutana kwenye mauzo yake, kabla ya hajaumia mguu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

  Leroy Sane anakwenda kujiunga na Bayern Munich kwa dau la Pauni Milioni 55 kutoka Manchester City 

  Tangu hapo, Sane amecheza mechi moja tu tena kwa dakika 11 tu katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Burnley wiki iliyopita.
  Sane anakwenda Bavaria kujiunga na kikosi cha Hans-Dieter Flick kwa mshahara wa Pauni 350,000 kwa wiki, lakini hatacheza Bayern hadi msimu ujao.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LEROY SANE ATUA BAYERN MUNICH KWA DAU LA PAUNI MILIONI 55 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top