• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 03, 2019

  SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUSHINDWA KUINUSURU KRC GENK KUPIGWA 2-0 UGENINI UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, EUPEN 
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana alitokea benchi kipindi cha pili klabu yake, KRC Genk ikichapwa 2-0 na AS Eupen katika mchezo wa ugenini wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Am Kehrweg, Eupen.
  Samatta aliingia dakika ya 58 kuchukua nafasi ya mshambuliaji mwenzake, Mnigeria Stephen Odey, wakati huo tayari AS Aupen inaongoza 2-0 kwa mabao ya Jonathan Bolingi dakika ya 20 na Jordi Amat dakika ya 23.
  Hata hivyo, Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ hakuweza kuinusuru Genk na kipigo cha tano cha msimu katika mchezo wa 13, hivyo inabaki na pointi zake 20, sasa ikizidiwa pointi 13 na vinara, Club Brugge.

  Samatta jana amecheza mechi ya ya 172 jumla kwenye mashindano yote tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa amefunga mabao 69.
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 135 na kufunga mabao 53, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja, Europa League mechi 24 na mabao 14 na Ligi ya Mabingwa Ulaya mechi tatu tu akiwa amefunga bao moja.
  Kikosi cha AS Eupen kilikuwa; De Wolf, Verdon, Amat, Blondelle, Beck, Ebrahimi, Cools, Schouteden, Milicevic/Embalo dk77, Bolingi/Koch dk63 na Bautista/Toyokawa dk87.
  KRC Genk; Coucke, Maehle, Cuesta, Lucumi, Wouters, Berge, Hrosovsky, Ndongala/Ito dk45, Bongonda/Hagi dk75, Onuachu na Odey/Samatta dk58.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI NA KUSHINDWA KUINUSURU KRC GENK KUPIGWA 2-0 UGENINI UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top