• HABARI MPYA

    Tuesday, November 05, 2019

    MWINYI ZAHERA ATUPIWA VIRAGO NA BENCHI LAKE ZIMA UFUNDI, MKWASA KOCHA TENA YANGA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    HATIMAYE klabu ya Yanga SC imeachana na kocha wake, Mwinyi Zahera raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kipindi cha miezi 15 na ushei tangu apewe nafasi hiyo.
    Uamuzi huo umetangazwa leo na Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk. Mshindo Msolla katika mkutano wake na Waandishi wa Habari mchana wa leo makao makuu ya klabu, Jangwani mjini Dar es Salaam na sasa kiungo na Nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ atakuwa kocha wa muda.
    “Tumefikia maamuzi kama Kamati ya Utendaji ya kuachana na benchi lote la ufundi la klabu ya Yanga. Maana yake ni nini, ni kwamba tumeachana salama na mwalimu Kocha Mkuu Zahera, salama na kocha Noel Mwandila na tutaachana salama na benchi lote la ufundi kaunzia Meneja mpaka mlinzi,”amesema Dk Msolla.

    Aidha, Mwenyekiti huyo wa Yanga amesema kwamba wamekubaliana katika kikao cha Kamati ya Utendaji kuanza upya na wafanyakazi wote wa benchi la Ufundi wameondolewa.
    “Maana yake ni kwamba tumeamua tuanze upya, kama mtu atarudi, atarudi kwa utaratibu mwingine, lakini kwa leo na maamuzi ya Kamati ni kwamba tuanze upya. Sasa tulikuwa na kikao kwanza na walimu ndiyo maana tumechelewa tulikuwa na walimu wote wawili, tuongea kila kitu, tumepitia mikataba, tumeridhiana na tunaendela na taratibu nyingine za kuachana salama,”amesema.
    Uamuzi unakuja siku mbili baada ya Yanga SC kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kufuatia kuchapwa 3-0 na wenyeji, Pyramids FC Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 mjini Cairo katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 5-1 kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza mjini Mwanza Jumapili wiki iliyopita.
    Zahera alijiunga na Yanga SC Mei mwaka jana akichukua nafasi ya Mzambia, George Lwandamina – na baada ya kuwa timu kwa miezi 15 bila kushinda taji lolote ameondolewa kwa pamoja na benchi lake zima la Ufundi.
    Aliyekuwa Msaidizi wake, Mzambia Noel Mwandila, Meneja Hafidh Saleh, Mtunza Vifaa, Mohamed Omar ‘Mpogolo’, Mchua Misuli, Jackob Onyango na Daktari Edward Bavu nao wanafuatana na bosi wao, wakati kipa wa makipa pekee Manyika Peter ndiye amependekezwa kubaki. 
    Katika kipindi cha miezi 15, Zahera ameiongoza Yanga katika jumla ya mechi 75 za kirafiki na mashindano, kati ya hizo akishinda 45, kufungwa 17 na sare 13.
    Msimu uliopita Yanga SC ilimaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu, nyuma ya Simba SC waliobuka mabingwa, wakati katika Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) ilitolewa katika Nusu Fainali na Lipuli FC ya Iringa.
    Msimu huu Yanga ilianzia katika Ligi ya Mabingwa Afrika na baada ya kuitoa Township Rollers ya Botswana kwa jumla ya mabao 2-1, ikitoa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kushinda 1-0 Gaborone, ikaenda kutolewa na Zesco United ya Zambia kwa jumla ya mabao 3-2, ikitoka sare ya 1-1 nyumbani na kwenda kufungwa 2-1 Ndola.
    Ndipo ikaangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na baada ya kutolewa na Pyramids FC amepoteza ajira
    Katika Ligi Kuu hadi sasa msimu huu, Yanga SC imecheza mechi nne na kushinda mbili, sare moja  na kufungwa moja pia.

    REKODI YA MWINYI ZAHERA YANGA
    Yanga SC 2-1 USM Alger (Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Taifa)
    Yanga SC 2-1 Mtibwa Sugar (Alikuwa jukwaani, Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 0-1 Rayon Sport (Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Kigali)
    Yanga SC 1-0 African Lyon (Alikuwa DRC na timu ya taifa, Kirafiki Taifa)
    Yanga SC 4-3 Stand United (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 1-0 Coastal Union (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-0 Singida United (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 0-0 Simba SC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-0 Mbao FC (Alikuwa DRC na timu ya taifa, Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-0 Malindi FC (Kirafiki Zanzibar, alikuwa DRC na timu ya taifa)
    Yanga SC 3-0 Alliance FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 1-0 KMC FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 1-0 Lipuli FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 1-1 Ndanda FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 1-0 African Lyon (Kirafiki Uhuru, alikuwa DRC na timu ya taifa)
    Yanga SC 1-1 Reha FC (Kirafiki Uhuru, alikuwa DRC na timu ya taifa) 
    Yanga SC 1-1 Namungo FC (Kirafiki Ruangwa, alikuwa DRC na timu ya taifa)
    Yanga SC 2-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Shinyanga)
    Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu Bukoba)
    Yanga SC 3-1 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Sokoine) 
    Yanga SC 1-2 Sumbawanga United (Kirafiki Sumbawanga) 
    Yanga SC 2-1 Biashara United (Ligi Kuu Taifa) 
    Yanga SC 3-2 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Taifa) 
    Yanga SC 1-0 African Lyon (Alikuwa safari Ufraansa, Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-1 Mbeya City (Ligi Kuu Sokoine) 
    Yanga SC 1-0 KVZ (Alibaki Dar, Kombe la Mapinduzi Zanzibar)
    Yanga SC 0-3 Azam FC (Alibaki Dar, Kombe la Mapinduzi Zanzibar)
    Yanga SC 1-2 Malindi SC (Alibaki Dar, Kombe la Mapinduzi Zanzibar)
    Yanga SC 3-1 Jamhuri FC (Alibaki Dar, Kombe la Mapinduzi Zanzibar) 
    Yanga SC 3-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Taifa) 
    Yanga SC 0-1 Stand United (Ligi Kuu Kambarage) 
    Yanga SC 2-3 Kariobangi Sharks (SportPesa Cup) 
    Yanga SC 2-2 (PENALTI 5-4) Biashara United (Kombe la TFF Taifa) 
    Yanga SC 1-1 Coastal Union (Ligi Kuu Mkwakwani) 
    Yanga SC 0-0 Singida United (Ligi Kuu Namfua) 
    Yanga SC 1-0 JKT Tanzania (Ligi Kuu Mkwakwani)
    Yanga SC 0-1 Simba SC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-1 Mbao FC (Ligi Kuu CCM Kirumba) 
    Yanga SC 1-0 Namungo FC (Kombe la TFF Taifa)
    Yanga SC 1-0 Alliance FC (Ligi Kuu CCM Kirumba) 
    Yanga SC 1-0 KMC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 0-1 Lipuli FC (Alikuwa DRC, Ligi Kuu Samora)
    Yanga SC 1-1 (Penalti 4-3) Alliance FC (Kombe la TFF Kirumba)
    Yanga SC 1-1 Ndanda FC (Ligi Kuu Nangwanda)
    Yanga 3-2 Kagera Sugar (Ligi Kuu Kirumba)
    Yanga 0-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Jamhuri, Morogoro)
    Yanga 1-0 Azam FC (Ligi Kuu Uhuru, Dar es Salaam)
    Yanga 2-1 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Uhuru, Dar es Salaam)
    Yanga 0-2 Lipuli FC (Kombe la TFF, Samora) 
    Yanga 0-1 Biashara United  (Ligi Kuu, Musoma) 
    Yanga 1-0 Ruvu Shooting  (Ligi Kuu, Uhuru) 
    Yanga 1-0 Mbeya City  (Ligi Kuu, Uhuru) 
    Yanga 0-2 Azam FC  (Ligi Kuu, Taifa) 
    Yanga SC 10-1 Tanzanite (Hakuwepo alikuwa likizo DRC)
    Yanga SC 7-0 ATN (Hakuwepo alikuwa likizo DRC)
    Yanga SC 2-0 Moro Kids (Hakuwepo alikuwa likizo DRC)
    Yanga SC 1-0 Mawenzi Market (Hakuwepo alikuwa likizo DRC)
    Yanga SC 1-1 Kariobangi Sharks (kirafiki Wiki ya Mwananchi)
    Yanga SC 4-1 Mlandege (kirafiki Zanzibar)
    Yanga SC 1-1 Malindi SC (kirafiki Zanzibar)
    Yanga SC 1-1 Township Rollers (Ligi ya Mabingwa Taifa)
    Yanga SC 0-2 Polisi Tanzania (Kirafiki Moshi)
    Yanga SC 1-0 AFC Leopards (Kirafiki Arusha)
    Yanga SC 1-0 Township Rollers (Ligi ya Mabingwa Gaborone)
    Yanga SC 0-1 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 1-1 Pamba SC (Kirafiki CCM Kirumba)
    Yanga SC 3-0 Toto Africans (Kirafiki Nyamagana)
    Yanga SC 1-1 Zesco United (Ligi ya Mabingwa Taifa)
    Yanga SC 1-2 Zesco United (Ligi ya Mabingwa Ndola)
    Yanga SC 3-3 Polisi Tanzania (Alikuwa jukwaani anatumikia adhabu, Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga SC 1-0 Polisi Tanzania (Alikuwa jukwaani anatumikia adhabu, Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga SC 1-0 Mbao FC (Alikuwa jukwaani anatumikia adhabu, Ligi Kuu Kirumba)
    Yanga SC 2-1 Pamba FC (Kirafiki asubuhi CCM Kirumba)
    Yanga SC 1-2 Pyramids FC (Kombe la Shirikisho CCM Kirumba)
    Yanga SC 0-3 Pyramids FC (Kombe la Shirikisho Cairo)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWINYI ZAHERA ATUPIWA VIRAGO NA BENCHI LAKE ZIMA UFUNDI, MKWASA KOCHA TENA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top