• HABARI MPYA

  Monday, November 04, 2019

  AZAM FC YAFIKISHA MECHI TATU BILA USHINDI LIGI KUU BAADA YA SARE YA 0-0 NA KAGERA SUGAR LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Huo unakuwa mchezo wa tatu mfululizo kwa Azam FC kucheza bila kushinda, kufuatia kufungwa 1-0 mara mbili mfululizo katika mechi za ugenini dhidi ya Simba SC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Na mechi zote hizo tatu imecheza chini ya Kocha Mromana, Aristica Cioaba aliyereshwa mwezi uliopita baada ya kuondolewa kwa Mrundi, Etienne Ndayiragijje ambaye amekwenda kuwa kocha wa kudumu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

  Mapema jioni katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu uliofanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, KMC iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Biashara United ya Musoma mkoani Mara.
  Mabao ya KMC inayofundishwa na kocha Mganda, Jackson Mayanja yamefungwa na Serge Tape dakika ya 30 na Kenny Ally dakika ya 58, wakati la Biashara United limefungwa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ dakika ya 65.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAFIKISHA MECHI TATU BILA USHINDI LIGI KUU BAADA YA SARE YA 0-0 NA KAGERA SUGAR LEO Rating: 5 Reviewed By: Mwakasege Blog
  Scroll to Top