• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 02, 2019

  KATIBU MKUU YANGA SC BADO NI KITENDAWILI, ATEULIWA MTU MWINGINE WA KUKAIMU, TEN…

  Na Mwandishi Wetu, DAR ESSALAAM
  KLABU ya Yanga imemteua Thabit Kandoro kuwa Kaimu Katibu Mkuu wake, nafasi ambayo imeachwa wazi na Dismas Ten aliyekuwa anakaimu pia.
  Uteuzi wa Kandoro uliotangazwa na Mwenyekiti, Dk. Mshindo Msolla umefuatia kuajiriwa kama Mkurugenzi wa Mashindano Yanga wa klabu hiyo.
  Dk. Msolla ambaye ni kocha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kwamba Ten ambaye awali alikuwa Afisa Habari sasa anahamishiwa kwenye nafasi ya Ofisa Masoko.

  Mbali na Kandoro, waajiriwa wengine wapya ni Simon Patrick anayekwenda kuwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Robert Kabeya anayekwenda kuwa Mkurugenzi wa Masoko.
  Tangu kujiuzulu kwa Charles Boniface Mkwasa Julai mwaka jana, watu wawili wamekwishakaimu nafasi ya Ukatibu Mkuu Yanga, akianza Omar Kaya kwa mwaka mmoja kabla ya kupokewa na Ten anayeondolewa sasa. 
  Mkwasa alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Yanga SC Januari 31, mwaka 2017,  akichukua nafasi ya Baraka Deusdedit ambaye wakati huo alirejeshwa kwenye Idara ya Fedha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KATIBU MKUU YANGA SC BADO NI KITENDAWILI, ATEULIWA MTU MWINGINE WA KUKAIMU, TEN… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top