• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 01, 2019

  SIMBA SC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA SEVILLA YA HISPANIA MEI 23 UWANJA WA TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza timu ya Simba ya Tanzania kucheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa na Sevilla ya Hispania Mei 23,2019 Uwanja wa Taifa.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo amesema kwamba Simba imetajwa kucheza mchezo huo dhidi ya Sevilla kwa kigezo cha Klabu ya Tanzania iliyofanya vizuri katika mashindano ya SportPesa Cup kwa timu zinazodhaminiwa na SportPesa.
  Sevilla waliopo kwenye Ligi Kuu ya Hispania La Liga wataingia Tanzania Mei 21,2019 tayari kwa mchezo huo.
  Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred amesema kigezo kikubwa kilichotumika kuchagua timu ya kucheza mchezo huo ni timu ya Tanzania iliyofanya vizuri katika mashindano ya SportPesa ambapo Simba ilifikia hatua ya nusu fainali.
  Amesema ratiba ya Ligi Kuu imebana kimetumika kigezo cha mashindano ya SportPesa kumpata muwakilshi wa kucheza na Sevilla.
  Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tarimba Abas awali kulikuwa na wazo la kuzikutanisha Simba na Young Africans ili kupatikana timu moja lakini ratiba imekuwa ngumu kuzikutanisha timu hizo au kuchezwa michezo mawili.
  Ameongeza kuwa kigezo cha kutumia mashindano ya SportPesa kinaondoa ugumu wa kupatikana timu ya kucheza na Sevilla. Tayari maandalizi kwaajili ya mchezo huo yanaendelea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA SEVILLA YA HISPANIA MEI 23 UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top