• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 20, 2017

  SAMATTA ASHINDWA KUIBEBA GENK NYUMBANI, YALAZIMISHWA SARE 1-1

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta jana ameshindwa kuisaidia timu yake, KRC Genk kupata ushindi nyumbani, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Charleroi SC katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, Ubelgiji.
  Dakika 45 za kwanza zilimalizika bila mabao na kipindin cha pili, wenyeji Genk wakatangulia kwa bao la penalti la Leandro Trossard dakika ya 84, kabla ya Stergos Marinos kuiswazishia Charleroi SC dakika ya 86.
  Mbwana Samatta alipambana sana, lakini akashindwa kuipa ushindi Genk nyumbani

  Samatta jana alicheza mechi yake ya 43 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 25 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 24 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 14 msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 12, sita msimu huu na sita msimu uliopita.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Castagne, Colley, Brabec/Castagne dk67, Berge, Malinovskyi/Boetius dk77, Pozuelo/Naranjo dk88, Trossard, Authors na Samatta.
  Charleroi SC: Penneteau, Martos, Harbaoui, Diandy, Benavente/Hendrickx dk56, Baby, Mata/Marinos dk79, Dessoleil, Marcq, N'Ganga na Bedia/Fall dk88.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ASHINDWA KUIBEBA GENK NYUMBANI, YALAZIMISHWA SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top