• HABARI MPYA

  Sunday, February 26, 2017

  SAMATTA AWEKEWA ULINZI ‘WA KUFA MTU’, GENK YAFA 2-0 KWA ANDERLECHT

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  USIKU wa leo, Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta atalala hoi baada ya dakika 90 za mechi ngumu ya Ligi Daraja la Kwanza A, timu yake, KRC Genk ikichapwa mabao 2-0 na wenyeji, RSC Anderlecht Uwanja wa Constant Vanden Stock mjini Brussels, Ubelgiji.
  Samatta aliwekewa ulinzi mkali katika mchezo huo wa ugenini, lakini na bado akawahenyesha mabeki wa Anderlecht kiasi kwamba  na wao watalala hoi.
  Mabao ya RSC Anderlecht yamefungwa na beki Msenegali, Serigne Modou Kara Mbodji dakika ya 32 na kiungo Mbelgiji, Yoeri Tielemans dakika ya 50.
  Mbwana Samatta (kushoto) chini ya ulinzi mkali wa wa mabeki wa Anderlecht leo

  Anderlecht inafikisha pointi 55 baada ya ushindi huo ikiwa imecheza mechi 27 na inaendelea kukaa nafasi ya pili, nyuma ya Club Brugge yenye pointi 58 za mechi 28, wakati Genk inabaki na pointi zake 42 za mechi 27 katika nafasi ya saba.  
  Leo Samatta amecheza mechi yake ya 45 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 27 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 26 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 16 msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 12, sita msimu huu na sita msimu uliopita.
  Kikosi cha RSC Anderlecht kilikuwa: Boeckx, Kara, Najar, Bruno/Stanciu dk84, Chipciu/Trebel dk64, Nuytinck, Thelin/Acheampong dk89, Tielemans, Dendoncker, Obradovic na Hanni.
  KRC Genk : Ryan, Castagne, Brabec, Colley, Uronen, Berge, Malinovskyi/Naranjo dk75, Pozuelo, Trossard/Boetius dk45, Writers/Buffalo dk64 na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AWEKEWA ULINZI ‘WA KUFA MTU’, GENK YAFA 2-0 KWA ANDERLECHT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top