• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 27, 2017

  YANGA KUPOZA MACUNGU KWA RUVU SHOOTING KESHOKUTWA?

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea keshokutwa Jumatano ambako mabingwa watetezi wa taji hilo, Yanga itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikitoka kufungwa mabao 2-1 na mahasimu wao wa jadi, Simba Jumamosi Uwanja wa Taifa katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu. 
  Mbali ya mchezo huo mmoja kwa siku ya Jumatano, ligi hiyo ambayo ni michuano mikubwa nchini, itaendelea mwishoni mwa wiki hii ambako kwa siku ya Jumamosi Machi 4, mwaka huu Simba itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Ukiacha mchezo huo, michezo mingine ya Jumamosi Machi 4, mwaka huu itakuwa ni kati ya Toto Africans na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza huku Kagera Sugar ikiikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Azam FC pia itacheza Jumamosi Machi 4, mwaka huu na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Chamazi. Mchezo huo utaanza saa 1.00 jioni wakati mechi nyingine zitaanza saa 10.00 jioni.
  Mtibwa Sugar itaialika Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Jumapili Machi 5, wakati African Lyon itaialika Mwadui ya Shinyanga na Ndanda FC itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA KUPOZA MACUNGU KWA RUVU SHOOTING KESHOKUTWA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top