• HABARI MPYA

  Tuesday, February 28, 2017

  LWANDAMINA AWATAKA WACHEZAJI YANGA KUSAHAU KIPIGO CHA SIMBA NA KUFIKIRIA UBINGWA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amewaambia wachezaji wake wasahau kipigo cha Simba Jumamosi na kuelekeza nguvu zao katika michezo ijayo ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Baada ya kufungwa 2-1 na Simba Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga kesho wanarejea uwanjani hapo, kumenyana na Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.  
  Akizungumza katika mahojiano maalum na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Lwandamina amesema kwamba maandalizi ya mchezo wa kesho yanaendelea vizuri. 
  George Lwandamina amewaambia wachezaji wake wasahau kipigo cha Simba Jumamosi na kuelekeza nguvu zao katika michezo ijayo

  “Wanatakiwa (wachezaji) kukiacha nyuma kipigo cha Simba na kauelekeza fikra zao katika mwchi zijazo,”alisema.
  Alipoulizwa kuhusu wachezaji beki Mtogo Vincent Bossou na mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma ambao walikosa mchezo wa Simba kwa maelezo kwamba ni majeruhi, lakini baadaye ikagundulika waligoma, Lwandamina alisema taarifa zao zipo kwa uongozi.
  Bossou na Ngoma wanadaiwa kugoma kwa madai wanaidai fedha klabu, lakini Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa jana kwamba wakati mshahahara wake wa Januari unatoka alikuwa Gambia na timu yake ya taifa, Togo kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
  “Tatizo mtu ambaye alikuwa ana cheki ya mshahara wa Januari wa Bossou (kutoka Quality Group) alitaka amkabidhi mchezaji mwenyewe cheki yake. Sasa Bossou amerejea anatakiwa kufuatilia mshahara wake Quality,”amesema Mkwasa.
  Pamoja na hayo, Mkwasa amesema Bossou alifanya mazoezi kikamilifu kabla ya mechi na Simba SC, lakini kwa taarifa zilizopo aliondoka kambini bila ruhusa ya mwalimu, hivyo wanasubiri ripoti ya mwalimu kwa ajili ya kumchukulia hatua.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LWANDAMINA AWATAKA WACHEZAJI YANGA KUSAHAU KIPIGO CHA SIMBA NA KUFIKIRIA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top