• HABARI MPYA

  Monday, February 27, 2017

  MLANDIZI QUEENS YAANZA VYEMA LIGI YA WANAWAKE BARA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya soka ya Wanawake Tanzania Bara, hatua ya timu sita Bora (6), ilianza rasmi jana kwa Mlandizi Queens ya Pwani kuilaza JKT Queens ya Dar es Salaam mabao 3-2 katika mchezo wa awali mchana kabla ya ule wa jioni Sisterz ya Kigoma kuifunga Fair Play ya Tanga mabao 5-1.
  Ligi hiyo inayochezwa Kituo kimoja cha Uwanja wa Karume, Ilala Dar es Salaam inakutanisha timu sita zinazowania ubingwa wa ligi hiyo ya wanawake ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania. Pia ni ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki.
  Timu sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.
  Mara baada ya mechi za jana Februari 26, 2017; ligi hiyo sasa itaendelea kesho Februari 28, mwaka huu ambako kwa michezo ifuatayo:   
  Februari 28, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Panama saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi na Fair Play.
  Machi 2, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Sisterz na Marsh Academy saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na JKT Queens.
  Machi 4, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na JKT Queens saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Mlandizi Queens.
  Machi 6, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Panama na Sisters saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Marsh Academy.
  Machi 8, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Sisters na Mlandizi Queens saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na Fair Play.
  Machi 10, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Fair Play saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi na Panama.
  Machi 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tu saa 10.00 jioni ambako JKT Queens watamaliza na Sisterz.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MLANDIZI QUEENS YAANZA VYEMA LIGI YA WANAWAKE BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top