• HABARI MPYA

  Tuesday, February 28, 2017

  ISRAEL NKONGO KUCHEZESHA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limeteua waamuzi wanne wa Tanzania watakaochezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu za AS Porto Louis 2000 ya Mauritius na El Hilal ya Sudan wikiendi ijayo.
  Katika mchezo huo ambao utafanyika ama Machi 17, 18 au 19 Mwamuzi wa kati atakuwa Israel Mujuni Nkongo wakati wasaidizi wake watakuwa ni Samuel Hudson Mpenzu na Josephat Deu Bulali huku Mwamuzi wa akiba akiwa ni Elly Ally Sasii.
  Kamisha katika mchezo huo Na. 78 atakuwa Jerome Kelvyn Damon kutoka Afrika Kusini.
  Israel Nkongo (kulia) ni miongoni mwa marefa wazoefu Tanzania na mwenye sifa za kuchezesha mechi kubwa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ISRAEL NKONGO KUCHEZESHA LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top