• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 28, 2017

  MAREFA WA DJIBOUTI KUCHEZESHA YANGA NA ZANACO TAIFA MACHI 11

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetaja marefa watakaochezesha mechi ya kwanza ya hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji, Yanga na Zanaco ya Zambia Machi 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  
  Marefa hao wanaotokea Djibouti ni Djamal Aden Abdi ambaye atapuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera, Hassan Yacin na Farhan Salime na mwamuzi wa akiba, Souleiman Djamal.
  Kamisaa katika mchezo huo namba 61 atakuwa Luleseged Asfaw kutoka Ethiopia.
  Amissi Tambwe anatarajiwa kuiongoza Yanga dhidi ya Zanaco ya Zambia Machi 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  Aidha, CAF pia imetaja waamuzi watakochezesha mchezo kati ya wenyeji Azam FC na Mbabane Swallows ya Swaziland Machi 12, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Hao ni Addissa Abdul Ligali atakayepuliza filimbi na washika vibendera Medegnonwa Romains Agbodjogbe na Babadjide Bienvenu Dina, wakati mwamuzi wa akiba akiwa Moumouni Kiagou wote kutoka Benin na kamisaa Mohamed Omar Yusud wa Kenya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAREFA WA DJIBOUTI KUCHEZESHA YANGA NA ZANACO TAIFA MACHI 11 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top