• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 25, 2017

  LWANDAMINA AWAANZISHWA PAMOJA YONDAN NA DANTE BEKI YA KATI YANGA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mambia wa Yanga, George Lwandamina amewanzisha pamoja Andrew Vincent ‘Dante’ na Kevin Yondan kucheza pamoja beki ya kati katika mchezo dhidi ya mahasimu, Simba.
  Watani wa jadi, Simba na Yanga wanavaana katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na Lwandamina amemuacha benchi Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ huku Mtogo, Vincent Bossou akiwa jukwaani kwa sababu ya maumivu ya nyonga.
  George Lwandamina ametupa karata yake kwa Andrew Vincent ‘Dante’ na Kevin Yondan katika beki ya kati leo

  Kikosi kamili cha Yanga kinachoanza ni; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Andrew Vincent, Kevin Yondan, Justine Zulu, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Obrey Chirwa na Haruna Niyonzima.
  Katika benchi wapo; wapo Ally Mustafa ‘Barthez’, Hassani Kessy, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Geoffrey Mwashiuya, Deus Kaseke na Juma Mahadhi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LWANDAMINA AWAANZISHWA PAMOJA YONDAN NA DANTE BEKI YA KATI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top