• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 22, 2017

  MKUTANO WA BARAZA KUU LA BODI YA LIGI FEBRUARI 26, 2017, MFUKO WA KUSAIDIA SERENGETI BOYS KUZINDULIWA KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MKUTANO wa Tatu wa Baraza Kuu la Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) chini ya Mwenyekiti wake Bw. Hamad Yahya Juma utafanyika Jumapili, Februari 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wa Mkutano huo wa mwaka 2016 ambao utaanza saa 4 asubuhi ni wenyeviti wa klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom, na klabu zote za Ligi Daraja la Kwanza.
  Ajenda za Mkutano huo ambazo zimeainishwa katika Ibara ya 21 ya Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi  Kuu ni Kuhakiki Akidi, Kufungua Mkutano, Kuthibitisha Ajenda, Kuthibitisha Muhtasari wa Mkutano Uliopita, Yatokanayo na Mkutano Uliopita, Hotuba ya Mwenyekiti, Taarifa ya Utendaji ya Kamati ya Uongozi, Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa, Kupitisha Bajeti, Mengineyo na Kufunga Mkutano.
  Wakati huo huo: Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kesho Februari 23, 2017 inatarajiwa kuzindua Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa miguu kwa vijana na wanawake.
  Uzinduzi huo utakaofanyika saa 5.00 asubuhi, utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mkurugenzi wa Michezo, Yussuph Singo. Utafanyika kwenye Ukumbi wa 
  Hoteli ya Courtyard, Upanga jijini Dar es Salaam.
  Mfuko huo uko chini ya Mwenyekiti Bw. Tido Mhando ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Azam Media wakati Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo ni Bw. Dereck Murusuri.
  Wajumbe wake ni Beatrice Singano, Ephraim Mafuru, Tarimba Abbas, Joseph Kahama, Salum Rupia na Meshack Bandawe.
  Majukumu ya Kamati ya Mfuko huo ni kukusanya rasilimali kwa ajili ya kuendeshea program za TFF za maendeleo ya mpira wa vijana wa wanawake.
  Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, mfuko huu ni huru, una sekretariet yake, akaunti yake benki na ofisi zake zinazotarajiwa kuwa Mikocheni, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MKUTANO WA BARAZA KUU LA BODI YA LIGI FEBRUARI 26, 2017, MFUKO WA KUSAIDIA SERENGETI BOYS KUZINDULIWA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top