• HABARI MPYA

  Friday, February 24, 2017

  RANIERI ATIMULIWA LEICESTER MIEZI TISA BAADA YA KUWAPA UBINGWA WA ENGLAND

  Mtaliano Claudio Ranieri anaondoka Leicester miezi tisa baada ya kuwapa taji la kihistoria la Ligi Kuu ya Ebgland

  KLABU ya Leicester City imechukua maamuzi magumu baada ya kumfukuza kocha wake, Mtaliano Claudio Ranieri jana.
  Ranieri anaondoka Leicester miezi tisa baada ya kuwapa taji la kihistoria la Ligi Kuu ya Ebgland.
  Wamiliki wa klabu hiyo, kutoka Thailand walijitokeza kumtetea kocha wao mapema mwezi huu wakisema anastahili kuendelea na kazi. 
  Alipewa 'sapoti' ya nguvu na mabosi wake hao, lakini baada ya timu kufungwa 2-1 na Seville katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kucheza mechi sita za Ligi Kuu ya England bila kufunga bao, Ranieri anaondolewa King Power. 
  Na tayari Leicester City imethibitisha kuachana na Mtaklianohuyo siku 298 baada ya kuwapa ubingwa wa England.
  Makocha Wasaidizi, Paolo Benetti na coach Andrea Azzalin pia wanaondoka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RANIERI ATIMULIWA LEICESTER MIEZI TISA BAADA YA KUWAPA UBINGWA WA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top