• HABARI MPYA

  Monday, February 27, 2017

  MAKOCHA WAZAWA WAIKACHA NAFASI YA UKOCHA GHANA

  LICHA ya kwamba hawana kocha tangu wamemaliza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Chama cha Soka Ghana hakina haraka kutafuta mwalimu mpya.
  Vyombo vya habari nchini humo vimetoa orodha ya makocha walioomba kumrithi Avram Grant, ingawa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa GFA amesema kwamba hawajaanza hata kupokea maombi.
  Akizungumza mjini Accra jana, Ibrahim Sannie Daara alisema; "Kamati Kuu ya FA itakutana wiki ijayo kuamua vigezo vya kutumia katika uteuzi wa kocha mpya. Pia kuangalia kwamba itafute mwalimu, au itangaze nafasi ya kazi,".
  Pia amethibitisha kwamba zaidi ya maombi 60 yamepokewa hadi sasa, lakini akakataa kutaja majina ingawa tu alikiri hakuna kocha mzawa wa Ghana katika orodha hiyo.
  "Sijaona wasifu wa kocha wa nyumbani bado katika orodha hiyo zaidi tu ya tetesi za kwenye vyombo vya habari hapa nyumbani."
  Mjadala pia wa kocha mzawa au wa kigeni ndiye apewe Black Stars nao umechukua nafasi kubwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKOCHA WAZAWA WAIKACHA NAFASI YA UKOCHA GHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top