• HABARI MPYA

    Friday, February 24, 2017

    SAMATTA, GENK WAWEKA REKODI ULAYA, WAIFUATA MAN UNITED 16 BORA EUROPA LEAGUE

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samata usiku wa jana ameiongoza timu yake, KRC Genk kutinga hatua ya 16 Bora michuano ya Europa League baada ya kuifungaa FC Astra Giurgiu ya Romania bao 1-0 Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
    Matokeo hayo yanaifanya Genk isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya wiki iliyopita kulazimisha sare ya 2-2 ugenini.  
    Bao la Genk katika mchezo wa jana uliochezeshwa na refa Mholanzi, Serdar Gozubuyuk lilifungwa na kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 67.
    Mbwana Samatta (kushoto) akimpongeza Alejandro Pozuelo baada ya kufunga bao pekee jana

    Na sasa Genk inakuwa moja ya timu tatu za Ubelgiji zilizotinga hatua ya 16 Bora michuano hiyo, nyingine ni Anderlecht na Gent, zinazoungana na Manchester United ya England, APOEL ya Cyprus, Copenhagen ya Denmark, Lyon ya Ufaransa, Borussia Monchengladbach, Schalke 04 za Ujerumani, Olympiacos ya Ugiriki, Roma ya Italia, Ajax ya Uholanzi, Krasnodar, Rostov za Urusi, Celta Vigo ya Hispania na Besiktas ya Uturuki.
    Ratiba ya 16 Bora itapangwa leo mchana na mechi za kwanza zitachewa Machi 9 na marudiano yatakuwa Machi 16, mwaka huu.
    Aidha, jana Samatta jana amecheza mechi yake ya 44 tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana, 18 msimu uliopita na 26 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 25 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 15 msimu huu.
    Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 10 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu huku akiwa amefunga jumla ya mabao 12, sita msimu huu na sita msimu uliopita.
    Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa: Ryan, Castagne, Colley, Brabec, Uronen, Berge, Malinovskyi/Boetius dk90, Pozuelo/Kumordzi dk89, Trossard, Authors/Buffalo dk76 na Samatta.
    FC Astra Giurgiu : Lung, Morais Alves, Săpunaru, Stan Seto/Ionita dk82 Mansaly, Lovin/Bus dk70 Budescu, Niculae/Florea dk67 na Teixeira.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA, GENK WAWEKA REKODI ULAYA, WAIFUATA MAN UNITED 16 BORA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top