• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 23, 2017

  BOCCO AANZA MDOGO MDOGO AZAM FC, KINGUE BADO BADO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Azam FC, John Raphael Bocco, jana ameanza mazoezi mepesi baada ya kupata ahueni ya maumivu ya misuli ya paja.
  Daktari Mkuu wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, aliiambia Bin Zubeiry Sports - Online jana kwamba Bocco aliyeumia Janauri 28 katika mchezo dhidi ya Simba Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kufunga bao pekee Azam wakishinda 1-0, anaweza kurejea uwanjani baada ya wiki mbili.
  Pamoja na hayo, Dk Mwankemwa alisema kiungo Mcameroon, Stephan Kingue ambaye aliumia kwenye mchezo huo huo dhidi ya Smba nyama za paja, naye ameanza mazoezi ya gym.
  John Bocco ameanza mazoezi mepesi jana baada ya kupata ahueni ya maumivu ya misuli ya paja 
  "Bocco ameanza mazoezi mepesi bado yupo chini ya uangalizi wangu huku na huenda akarejea uwanjani baada ya wiki mbili kuanzia sasa,"alisema Mwankemwa.
  Mbali na Bocco, pia mtaalamu huyo amegusia hali ya kiafya ya Kingue akisema kuwa kiungo huyo tatizo lake limeonekana kuwa kubwa tofauti na Bocco na kudai huenda akarejea uwanjani baada ya wiki nne kuanzia sasa.
  “Unajua mwili wa binadamu ni tofauti na gari, gari likiharibika inachukua muda mfupi kuweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida, lakini mwili wa binadamu unahitaji tiba ya uhakika na muda kuweza kurejea kwenye hali ya kawaida,” alisema.  
  Kikosi cha Azam FC hivi sasa kipo kwenye maandalizi makali kuelekea mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Ijumaa kuanzia Saa 10.30 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BOCCO AANZA MDOGO MDOGO AZAM FC, KINGUE BADO BADO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top