• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 24, 2017

  MAN UNITED YAPELEKWA URUSI 16 BORA EUROPA LEAGUE, SAMATTA...

  Manchester United ya Jose Mourinho itamenyana na Rostov ya Urusi katika hatua ya 16 Bora michuano ya Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  RATIBA 16 BORA EUROPA LEAGUE 

  Celta Vigo vs Krasnodar
  APOEL vs Anderlecht
  Schalke vs Borussia Monchengladbach
  Lyon vs Roma
  Rostov vs Manchester United
  Olympiacos vs Besiktas
  Gent vs Genk
  Copenhagen vs Ajax 
  VIGOGO wa England, Manchester United watamenyana na Rostov katika hatua ya 16 Bora michuano ya Europa League.
  United iliingia hatua ya 16 kwa kishindo, baada ya kuitandika jumla ya mabao 4-0 St Etienne katika raundi ya kwanza ya mchujo.
  Mechi mbili zitachezwa kati ya Machi 9 na Machi 16, mwaka huu baina ya timu hizo. Timu ya Jose Mourinho watakuwa safari ngumu ya Urusi, siku nne kabla ya kukutana na Chelsea katika Robo Fainali ya Kombe la FA. 
  KRC Genk ya Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta imeangukia kwa wapinzani wao wa Ubelgiji, Gent, wakati Schalke itamenyana na wapinzani wao wa Bundesliga, Borussia Monchengladbach.
  Mechi nyingine Celta Vigo ya Hispania itamenyana na Krasnodar, APOEL ya Cyprus na Anderlecht ya Ubelgiji, Lyon ya Ufaransa na Roma ya Italia, Olympiacos ya Ugiriki na Besiktas ya Uturuki na Copenhagen ya Sweden dhidi ya Ajax ya Uholanzi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAPELEKWA URUSI 16 BORA EUROPA LEAGUE, SAMATTA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top