• HABARI MPYA

  Sunday, February 19, 2017

  YANGA KAMBINI LABDA KESHO, LEO PIA WANALALA NYAMWEZI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  YANGA SC inaweza kuingia kambini kesho, lakini bado haijajulikana wapi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya watani wa jadi, Simba SC Jumamosi ijayo.
  Mabingwa hao wa nchi, watakutana na mahasimu wao wa jadi, Simba SC Jumamosi wiki ijayo katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na wakati mahasimu wao waliwasili visiwani Zanzibar jana kuweka kambi, wao bado haijajulikana watakwenda wapi, ingawa kisiwa cha Pemba kinapewa nafasi kubwa zaidi.
  Wachezaji wa Yanga na Ngaya wakiingia uwanjani kwa ajili ya mchezo wa jana

  Kisiwa cha Pemba kimekuwa na bahati kwa Yanga, kila wanapokwenda kujificha huko hupata matokeo mazuri dhidi ya mahasimu wao, tofauti na wanapokwenda Bagamoyo au sehemu nyingine.
  Kwa sasa, kikosi cha Yanga kipo katika hoteli ya Zimbo, Mtaa wa Nyamwezi, Kariakoo mjini Dar es Salaam ambako kilijificha kwa ajili ya mchezo wa jana dhidi ya Ngaya Club de Mde ya Comoro.
  Yanga SC imefuzu raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Ngaya Club de Mde jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Imefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-2, baada ya Jumapili iliyopita kushinda 5-1 ugenini mjini Moroni, Comoro.
  Jana Ngaya ndiyo waliokuwa wa kwanza kuepata bao dakika ya 19 kupitia kwa Zahir Mohammed aliyefuua shuti baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Yanga na mpira ukampita kipa namba moja Tanzania, Deo Munishi ‘Dida’.
  Yanga ilisawazisha bao hilo dakika ya 43 kupitia kwa beki wa kushoto Mwinyi Hajji Mngwali, aliyefumua shuti kali kutoka umbali wa mita 25, baada ya pasi ya Kevin Yondan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KAMBINI LABDA KESHO, LEO PIA WANALALA NYAMWEZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top