• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 23, 2017

  CAF YATAJA VIKOSI VYOTE AFCON YA U-20 ZAMBIA 2017

  Wachezaji wa Cameroon wakiwa kwenye ndege kuelekea Zambia tayari kwa michuano hiyo 

  WAKATI michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 inaanza wikiendi hii nchini Zambia, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetaja vikosi vya timu zote.
  Michuano hiyo ya 20 inatarajiwa kuanza Jumapili wiki hii hadi Machi 12, mwaka huu na CAF imetaja vikosi vya timu zote nane zilizofuzu fainali za mwaka huu.
  Ikumbukwe timu zitakazoingia Nusu Fainali zitajihakikisia tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia za U-20 kuanzia Mei 10 hadi Juni 11 mwaka huu Jamhuri ya Korea.
  Kundi A mechi zake zitachezwa Lusaka, likihusisha timu za wenyeji, Zambia, Misri, Mali na Guinea, wakati Kundi B lina Afrika Kusini, Senegal, Cameroon na Sudan na watacheza mechi zao mjini Ndola.
  GONGA HAPA KUTAZAMA VIKOSI VYOTE 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAF YATAJA VIKOSI VYOTE AFCON YA U-20 ZAMBIA 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top