• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 21, 2017

  NGOMA SASA SI WA KUMTARAJIA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga, Donald Dombo Ngoma wa Zimbabwe ndiye mchezaji pekee kwenye kikosi hicho ambaye anaweza kukosekana kwenye mchezo dhidi ya mahasimu, Simba Jumamosi.
  Yanga watamenyana na mahasimu wao wa jadi, Simba Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Na kuelekea mchezo huo, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kwamba Ngoma ndiye majeruhi pekee aliyesalia katika timu, baada ya kupona kwa Amissi Joselyn Tambwe.
  Donald Ngoma mbele ya Daktari wa Yanga, Edward Bavu baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Stand United Februari 3, mwaka huu
  Meneja wa Yangam Hafidh Saleh amesema wachezaji wengine wote wapo fiti Yanga

  “Tambwe yuko fiti na Niyonzima (Haruna) aliyekuwa anasumbuliwa na Malaria pia, naye yuko fiti, kwa sasa mchezaji pekee ambaye hayuko fiti ni Ngoma, anayesumbuliwa na maumivu ya goti,”alisema Hafidh.  
  Mabingwa hao watetezi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wameweka kambi Kigamboni, Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo huo, wakati mahasimu wao Simba wapo Zanzibar.
  Kihistoria Kigamboni ni sehemu nyingine yenye kumbukumbu nzuri kwa Yanga, kwani kila ilipokuwa ikiweka kambi huko ilikuwa ikiwafunga mahasimu.
  Mwaka 1999 Yanga ilishinda mechi zote za Ligi dhidi ya Simba, 3-1 na 2-0 ikiwa inatokea Chuo cha Sayansi ya Jamii (sasa Chuo cha Mwalimu Nyerere), Kigamboni ilipoweka kambi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGOMA SASA SI WA KUMTARAJIA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top