• HABARI MPYA

    Thursday, February 23, 2017

    RAIS MALINZI AELEZA MIKAKATI WA MAENDELEO YA SOKA YA VIJANA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi ameelezea mikakati mbalimbali ya maendeleo ya soka nchini akisema hiyo ndiyo sababu ya Kamati ya Utendaji kubuni na kuunda Mfuko wa Maendeleo ya soka.
    Katika Risala yake aliyoitoa leo katika uzinduzi wa mfuko huo, Rais Malinzi alisema wamefanya hivyo kwa lengo la kutimiza ndoto za Tanzania kushiriki michuano mbalimbali ya soka.
    “Kwa kipindi kirefu Tanzania hatujafanikiwa kucheza fainali kubwa za mpira Barani Afrika. Mara ya mwisho kupata mafanikio makubwa kwa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ilikuwa ni mwaka 1980 Tanzania ilipofuzu kucheza fainali za Afrika (AFCON) nchini Nigeria,” amesema Rais Malinzi na kuongeza:
    “Ila kuhakikisha Tanzania inang’ara tena Kimataifa katika mpira wa miguu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linania thabiti ya kuhakikisha Tanzania inafuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mwaka 2026 kwa upande wa wanaume (Taifa Stars) na kufuzu kucheza fainali za Dunia kwa mpira wanawake (Twiga Stars) nchini Ufaransa mwaka 2019.
    “Msingi mkubwa wa mafanikio ya Timu za Taifa duniani kote ni kuwekeza katika mpira wa vijana ili kuhakikisha vijana wanafundishwa mpira kwa kiwango cha Kimataifa kuanzia wakiwa wadogo. Wakilelewa pamoja na kufundishwa mpira pamoja ukubwani wanaunda Timu ya Taifa imara yenye uwezo wa kushindana na timu yoyote duniani. Hakuna njia ya mkato,” alisisitiza Rais Malinzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS MALINZI AELEZA MIKAKATI WA MAENDELEO YA SOKA YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top