• HABARI MPYA

  Jumapili, Februari 19, 2017

  NI CHELSEA NA MAN UNITED ROBO FAINALI KOMBE LA FA

  Chelsea itakuwa mwenyeji wa kocha wake wa zamani, Jose Mourinho anayefundisha Manchester United kwa sasa

  RATIBA YA ROBO FAINALI KOMBE LA FA

  Chelsea vs Manchester United
  Middlesbrough vs Manchester City au Huddersfield
  Tottenham vs Millwall
  Sutton au Arsenal vs Lincoln
  Mechi zote zitachezwa wikiendi ya Machi 11 
  TIMU ya Lincoln City itamenyana na mshindi kati ya Sutton United na Arsenal katika Robo Fainali ya Kombe la FA England.
  Chelsea watakuwa wenyeji wa Manchester United katika mechi nyingine ya Robo Fainali ya michuano hiyo. 
  Mashabiki wa Imps walianza kuimba kwa furaha baada ya ratiba kupangwa ukumbi wa Travis Perkins Suite, Sincil Bank na kujua watacheza na timu ya Arsene Wenger, Gunners. 
  "Tunakuja kwako, tunakua kwako, Arsene Wenger, tunakuja kwako,"waliimba.
  The Imps wanakuwa timu ya kwanza isiyocheza Ligi yoyote kufika Robo Fainali ya Kombe la FA tangu mwaka 1914 walipoitoa Burnley. 
  Bao la ushindi la dakika ya 89 la Sean Raggett lilitosha kuipeleka timu hiyo yenye mashabiki 3,200 ugenini Uwanja wa Turf Moor.
  Middlesbrough watamenyana na Manchester City au Huddersfield, Tottenham na Millwall na mechi zote za Robo Fainali zinatarajiwa kuchezwa wikiendi ya Machi 11, mwaka huu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI CHELSEA NA MAN UNITED ROBO FAINALI KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top