• HABARI MPYA

  Thursday, February 23, 2017

  SIMBA YAMTIA MOTO MAVUGO AWAUE YANGA JUMAMOSI, YAMPA UCHEZAJI BORA WA JANUARI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KIASI cha siku tatu kabla ya kupambana na mahasimu wa jadi, Yanga – klabu ya Simba imemjenga kisaikolojia mshambuliaji wake, Mrundi Laudit Mavugo kwa kumtangaza Mchezaji Bora wa klabu wa mwezi Janauri.
  Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba Mavugo ndiye mchezaji bora wa klabu kwa Januari na atapatiwa Sh. 500,000 na taji kwa ushindi huo.
  Kwa sasa Simba ipo kambini kisiwani Zanzibar ikijiandaa na mchezo wa Jumamosi dhidi ya mahasimu, Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mrundi Laudit Mavugo ndiye Mchezaji Bora wa Simba SC kwa mwezi Janauri

  Mchezo huo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, unafuatia ule wa mzunguko wa kwanza, ambao timu hizo zilitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa pia Oktoba 1, mwaka jana.
  Yanga wao wameweka kambi eneo la Kimbiji, Kigamboni, Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAMTIA MOTO MAVUGO AWAUE YANGA JUMAMOSI, YAMPA UCHEZAJI BORA WA JANUARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top