• HABARI MPYA

    Friday, October 02, 2015

    LIVERPOOL, SPURS ZOTE ZASHINDWA KUFURUKUTA ULAYA

    LIVERPOOL imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na FC Sion usiku wa jana katika mchezo wa Kundi B michuano ya UEFA Europa League.  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Anfield, Liverpool ilitangulia kwa bao la Adam Lallana dakika ya nne kabla ya Ebenezer Assifuah kuwasawazishia wageni dakika ya 17.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Rubin Kazan imelazimishwa sare ya 0-0 na Bordeaux Uwanja wa Kazan Arena.
    Kundi J, Monaco imelazimishwa sare ya 1-1 na Tottenham Hotspur Uwanja wa Louis II. Spurs walitangulia kwa bao la Erik Lamela dakika ya 35 kabla ya wenyeji kusawazisha kupitia kwa Stephan El Shaarawy dakika ya 81.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, FK Qarabag imeshinda 1-0 dhidi ya RSC Anderlecht, bao pekee la Richard Almeida de Oliveira dakika ya 36 Uwanja wa Tofik Bakhramov.
    Beki wa kulia wa Liverpool, Nathaniel Clyne akimtoka mchezaji FC Sion, Carlitos jana Uwanja wa Anfield PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Kundi A, Molde imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ajax Uwanja wa Aker, nao lake likifungwa na Eirik Hestad dakika ya saba kabla ya wageni kusawazisha dakika ya 18 kupitia kwa Viktor Fischer.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Celtic imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Fenerbahce. Mabao ya Celtic yamefungwa na Leigh Griffiths dakika ya 28 na Kristian Commons daklika ya 32, wakati ya Fenerbahce yamefungwa na Jose Fernando Viana de Santana dakika ya 43 na 48 Uwanja wa Celtic Park.
    Kundi E; Villarreal wameshinda 1-0 dhidi ya Viktoria Plzen, bao pekee la Leonardo Carrilho Baptistao dakika ya 54 Uwanja wa El Madrigal, wakati mchezo mwingine wa kundi hilo, Dinamo Minsk wamefungwa 1-0 nyumbani na SK Rapid Wien, bao pekee la Steffen Hofmann dakika ya 54.
    Kundi F; Marseille imefungwa pia nyumbani 1-0 na Slovan Liberec, bao pekee la Vladimir Coufal dakika 84 Uwanja wa Velodrome, wakati Sporting Braga imeshinda 1-0 dhidi ya FC Groningen bao pekee la Ahmed Hassan dakika ya tano Uwanja wa 
    Manispaaa wa Braga.
    Kundi C; PAOK Salonika imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Borussia Dortmund Uwanja wa Toumba, bao likifungwa na Robert Mak dakika ya 34, wakati la wapinzani limefungwa na Gonzalo Castro dakika ya 72.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, FK Krasnodar imeshinda 2-1 dhidi ya FK Qabala Uwanja wa Kuban mabao yake yakifungwa na Wanderson do Carmo Carneiro dakika ya nane na Fedor Smolov dakika ya 84, la wapinzani wao likifungwa ma Luiz Paulo Hilario dakika ya 51.
    Kundi I, Fiorentina imeshinda 4-0 ugenini dhidi ya Belenenses mabao ya Federico Bernardeschi, Khouma Babacar, Antonio Leonel Nogueira Souza aliyejifunga na Giuseppe Rossi Uwanja wa Estadio do Restelo.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, FC Basel wameshinda 2-0 dhidi ya Lech Poznan, mabao ya Birkir Bjarnason na Breel Embolo kipindi cha pili Uwanja wa St Jakob-Park.
    Napoli imeshinda 2-0 ugenini katika mchezo wa Kundi D dhidi ya Legia Warsaw, mabao ya Dries Mertens na Gonzalo Higuain Uwanja wa Pepsi Arena, wakati mchezo mwingine wa kundi hilo,
    FC Midtjylland imeshinda 3-1 ugenini dhidi ya Club Brugge Uwanja wa Jan Breydelstadion.
    Mabao ya FC Midtjylland yamefungwa na Pione Sisto, Ebere Paul Onuachu na Filip Novak, wakati bao la wenyeji limefungwa na Thomas Meunier. Kundi K; FC Schalke 04 imeshinda 4-0 nyumbani dhidi ya Asteras Tripolis, Franco Di Santo akifunga mabao matatu peke yake dakika za 28, 37 na 44 kwa penalti, huku bao lingine likifungwa na Klaas-Jan Huntelaar dakika ya 84 Uwanja wa  
    VELTINS-Arena.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Sparta Prague imeshinda 2-0 dhidi ya APOEL Nicosia Uwanja wa Jenerali Arena, mabao yake yakifungwa na Kehinde Fatai dakika ya 24 na Jakub Brabec dakika ya 60.
    Kundi G, Lazio imeshinda 3-2 nyumbani dhidi ya St Etienne Uwanja wa Olimpico, mabao yake yakifungwa na Ogenyi Onazi dakika ya 22, Wesley Hoedt dakika ya 48 na Lucas Biglia dakika ya 80, huku ya wapinzani wao yakifungwa na Moustapha Bayal Sall dakika ya sita na Kevin Monnet-Paquet dakika ya 84.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Dnipro Dnipropetrovsk imeshinda ugenini 1-0 dhidi ya Rosenborg, bao pekee la Evgen Seleznyov dakika ya 79 Uwanja wa Lerkendal.
    Besiktas imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Sporting Lisbon katika mchezo wa Kundi H Uwanja wa Ataturk Olumpic. Bao la Besiktas limefungwa na Gokhan Tore dakika ya 61 wakati Sporting limefungwa na Bryan Ruiz dakika ya 16.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Lokomotiv Moscow imeshinda 2-0 dhidi ya Skenderbeu Korce Uwanja wa Lokomotiv, mabao ya Oumar Niasse na 
    Aleksandr Samedov.
    Kundi L, Partizan Belgrade imeshinda 3-1 ugenini dhidi ya FC Augsburg Uwanja wa WWK Arena mabao yake yakifungwa na Andrija Zivkovic dakika ya 31 na 62 na Fabricio Silva Dornellas dakika ya 54, la wenyeji likifungwa na Raul Bobadilla dakika ya 57.

    Mchezo mwingine wa kundi hilo, AZ imeshinda 2-1 nyumbani dhidi ya Athletic Club. Mabao ya AZ yamefungwa na Markus Henriksen dakika ya 55 na Eneko Boveda Altube la kujifunga dakika ya 65, wakati la wageni limefungwa na Aritz Aduriz Zubeldia dakika ya 75 Uwanja wa AFAS.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL, SPURS ZOTE ZASHINDWA KUFURUKUTA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top