• HABARI MPYA

    Tuesday, May 12, 2015

    RWANDA YASONGA MBELE OLIMPIKI, SASA KUIVAA UGANDA, KENYA YATOLEWA NA BOTSWANA

    TIMU ya taifa ya Rwanda imeungana na Botswana kwenda Raundi ya Pili ya mechi za kufuzu kwenye Fainali za vijana Afrika chini ya umri wa miaka 23, zitakazofanyika nchini Senegal baadaye mwaka huu 2015.
    Hiyo inafuatia Nyigu wa Kigali kulazimisha sare ya 1-1 na Somalia nchini Djibouti Jumapili, matokeo ambayo yanawafanya wasonge mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1 baada ya ushindi wa 2-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani.

    Rwanda, ambayo haijawahi kufuzu kwenye Michezo ya Olimpiki, sasa itamenyana na jirani zao upande wa kaskazini, Uganda katika hatua inayofuata, ambayo itazalisha timu saba za kuungana na wenyeji Senegal kwa fainali za michuano hiyo baadaye mwaka huu.
    Amavubi ndiyo waliotangulia kupata bao katika mchezo huo kupitia kwa Isaie Songa dakika ya nne, kabla ya Abbas Mohamed kuisawazishia Somalia dakika ya 60.
    Katika mchezo mwingine, Kenya nao walitupwa nje licha ya ushindi wa mabao 4-1 Jumamosi dhidi ya Botswana mjini Nairobi na kupoteza ndoto za kwenda Olimpiki ya Rio de Janeiro mwaka 2016.
    Matokeo hayo yanafanya sare ya jumla ya 4-4, baada ya Pundamilia kuwafunga Harambee Stars 3-0 katika mchezo wa kwanza, lakini Botswana inasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini kuhesabiwa mawili.
    Mshambuliaji Michael Olunga alipiga hat-trick katika mchezo huo, huku bao lingine la Kenya likifungwa na John Ndirangu wakati bao la Botswana lilifungwa Omaatlo Kebatho. 
    Botswana sasa watamenyana na ndugu zao wa Kusini mwa Afrika, Zambia.
    Timu tatu za juu katika fainali hizo za U-23 Afrika zinazotarajiwa kuanza Novemba 28 hadi Desemba 12 mwaka 2015 zitaliwakilisha bara hili katika Olimpiki ya mwakani mjini Rio de Janeiro, Brazil.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RWANDA YASONGA MBELE OLIMPIKI, SASA KUIVAA UGANDA, KENYA YATOLEWA NA BOTSWANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top