• HABARI MPYA

    Wednesday, May 27, 2015

    WAZIRI ATAKA MALAWI WASHIRIKI KOMBE LA MAPINDUZI

    Na Ali Issa, ZANZIBAR
    WAZIRI wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar, Said Ali Mbaruok amesema ushirikiano katika Nyanja za utalii,utamaduni na michezo ndio njia pekee ya kukuza uhusiano uliopo kati ya Nchi ya Zanzibar na Malawi
    Hayo ameyasema huko Wizara ya Habari  Utamaduni ,Utalii na Mchezo wakati alipokutana na Balozi mpya wa Malawi Nchini Tanzania Bi Hawa O.Ndilowe alipofika ofisini hapo kwa kujitambulisha kwa waziri huyo.
    Amesema ushirikiano huo utafanya mataifa yao kutembeleana katika Nyanja hizo na kubadilisha mawazo na kuongeza uhusiano wao unaimarika kwa kukutana mara kwa mara.
    Michuano ya Kombe la Mapinduzi hufanyika Januari kila mwaka na Simba SC ndio mabingwa watetezi upande wa soka

    “Tumekuwa na mashindano ya Kombe la Mapinduzi kila mwaka na nchi mbalimbali ambazo zinashiriki ni vyema Malawi nayo ikashiriki katika kombe hilo na ushirikiano wetu utakuwa zaidi”alisema Waziri Said.
    Aidha Waziri huyo amesema kuwa kwa vile Malawi imepiga hatua kimaendeleo katika masuala ya utalii michezo na Utamaduni itakuwa ni faraja kubwa kushirikiana katika njia hizo na kuona Zanzibar nayo inasonga mbele katika nyanja hizo.
    Waziri Mbarouk amemshukuru balozi huyo na kumtaka kufanya ziara nyengine ya kuitembelea Zanzibar pamoja na familia yake kwa  kujionea sehemu mbalimbali za vivutio vya kiutalii na kihistoria.
    Naye Balozi Ndilowe amemshukuru Waziri kwa mapokezi hayo na kusema kuwa ushirikiano wa Malawi na Zanzibar ni ushirikiano wa muda mrefu,hivyo kushirikiana katika masuala ya utalii, utamadu na michezo ni kukuza uhusiana wao uliopo.
    Amesema atazishawishi nchi nyengine pamoja na wageni mbalimbali kuja kutembelea Zanzibar katika Nyanja tofauti kwa lengo la kuleta maendeleo ya nchi na Mataifa yao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI ATAKA MALAWI WASHIRIKI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top