• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 25, 2015

  BURIANI MSHINDO MKEYENGE, BI NYAKOMBA, LAKINI...

  Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
  NI UKWELI kuwa mimi siyo mkongwe sana katika Tasnia ya Habari lakini ni Ukweli kuwa Nilianza kufuatilia masuala yanayohusu uandishi wa Habari Nikiwa Mdogo sana na kabla hata sijaanza shule ya Msingi.
  Mara Kwa mara Nilikuwa nasoma magazeti yaliyokuwa yakiletwa na Baba yangu,cha ajabu nilianza shule nikiwa najua kusoma kwakuwa tayari nilikuwa nasoma magazeti.
  Nilikuwa silali bila kuwa na Radio pembeni,ingawa Mama alikuwa Mkali akikataa nilale na Radio wakati wote. Si hivyo tu Nilikuwa na Radio Ndogo ambayo nilikuwa naiweka katika Begi la Shule na kwenda nayo shuleni huku tukiskiliza mimi Rafiki yangu Issa Hamisi.
  Kadiri Nilivyokuwa nasonga mbele kimadarasa ndivyo nilivyokuwa nazidi kupata upeo mkubwa kuhusiana na masuala ya Nchi yetu ya Tanzania kwa ujumla.
   Wakati Fulani Mama yangu alikuwa akinifukuza Ndani na kunambia nikacheze na Wenzangu baada ya kuona nakaa ndani muda mrefu tena nikiwa najifungia.

  Mtangazaji maarufu wa mpira wa zamani wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), sasa TBC, marehemu Mshindo Mkeyenge (katikati) akipokea tuzo yake ya heshima kutoka gazeti la Mwanaspoti usiku wa jana ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam Septemba mwaka juzi. 

  Lakini nilikuwa sijifungii ndani kwa nia mbaya `laa hasha!! Bali nilikuwa naskiza Radio na kusoma magazeti na vitabu ambavyo nilikuwa naiba chumbani kwa Baba.
   Siku moja Niliiba Kanda ya Maigizo nikawa naskiliza ingawa mara nyingi nilikuwa napenda kusikiza  Radio na siyo tep. Nikaskia sauti za akina Mzee Jongo wakiigiza Nyakati za siku kuu ya Idy  . Mzee Jongo alikuja na Wageni huku mkewe `Bi Nyakomba akiwa ameandaa Pilau nzuri mahsusi kwaajili ya Wageni.
  Kwa bahati mbaya Pilau ile ilimwagika hivyo ikawa tafrani. Sikunyingine Baba yangu alituwekea Kanda ya Mzee kipara na wenzake Igizo lilihusu kijana aliyepata cheo kikubwa na akatembelewa na Baba yake aliyetoka Kijijini,Baba alipofika Mjini akakuta mwanae anaishi maisha mazuri na Jumba la kifahari.
  Kwa bahati mbaya  Yule Mke wa kijana hakumpennda Baba mkwe,bila sababu za msingi.
   Kawa anamsingizia Baba mkwe kuwa ni mdokozi,mwizi anayeiba hela Ndani na Kijana akakubaliana na mkewe kasha kumpiga Baba yake ni kumfukuza. Mwishoe kijana akapata uwendawazimu na kazi akafukuzwa na maisha yakaharibika.iliifundisha jamii namna ya kuheshimu wazazi na kuwatunza. Ingawa fadhila zao hazilipiki.
  Mbali na hilo Nilikuwa mfuatiliaji sana wa Radio na Vyombo vyote vya habari kiasi chakuwashangaza Ndugu na jamaa na Ndiyo maana baada ya kumaliza shule nikaingia Uandishi wa Habari waliyokuwa wakinijua hawakushangaa.
  Kwa bahati mbaya sana baadhi ya waandishi wenzangu wa Habari wa kizazi hiki na hata kizazi kilichopita ambao bado ni waandishi siyo wenye urahibu wa kuhifadhi kumbukumbu na kuhangaisha akili kujua historia ya watu mbalimbali wenye mchango kwa Taifa hili.
  Mshindo Mkeyenge ,Mtangazaji Maarufu na miongoni mwa watangazaji wa kwanza Tanzania amefariki Dunia Nyumbani Kwake Temeke Dar es salaam, pia aliwahi kuwa Kiongozi wa Timu ya Soka Yanga.
  Kabla hajafariki Dunia,Mwishoni mwa mwaka juzi nilimfuata Nyumbani  kwake na kwenda kufanya mahojiano kuhusiana na Utangazaji wa Soka ambaye yeye ni alikuwa ni  `Fundi sana`.
   Alikuwa ameshakatwa Mguu kutokana na Maradhi yaliyokuwa yamemsibu. Aliongea Mengi na nikifikiria kuwa Ndiye huyu Mtangazaji mahiri wa Soka ambaye alianza kutangaza Soka nikiwa sijazaliwa huku Baba yangu akinipa historia yake kuwa alikuwa mtangazaji mahiri!!!!!
  Niwashukuru TASWA ambao waliwahi kumpa heshima ya Tunzo(  AHSANTENI) Nakumbuka siku hiyo ilikuwa Mlimani City na Mzee Mkeyenge akajibu kutangaza Mpira,watu walicheka na Kufurahi sana.( BINAFSI NILIFURAHI SANA TENA NIKIWA PEKE YANGU)
    Shirika la Utangazaji TBC huwa linarudia baadhi ya vipindi vya zamani sana,vingine hata sijazaliwa mimi, siku moja nadhani ni Miezi sita iliyopita Nyakati za Usiku wa saa saba hivi nikiwa naskiza Radio Tanzania ( sasa tbc Taifa) nikasikiza Mshindo Mkyenge akimuhoji Gwiji wa Taarab Al-Mar-hum Juma bhalo.
  Nikavutika kusikia kipindi hicho kwa umakini mkubwa,akamuuliza maswali kadha wa kadha Juma Bhalo na siku hiyo ndipo nilipobaini kumbe Juma Bhalo alizaliwa Somalia na Kukulia Mombasa!! Kumbe aliishi Tang asana!!
  Nilirekodi kipindi hicho na ninacho. Hivi jana tulipokuwa tukimzika Mzee Mkeyenge,Mtu aliyekuwa na historia pana katika utangazaji, waandishi wa Habari hawakuzidi watatu. Kusababu nyingi zilizofanya kutokeea kwa jambo hilo
  Kwa mtanzamo wangu sababu mojawapo ni waandishi wengi wa sasaivi kutokumfahamu Mshindo Mkeyenge nahii yote husababishwa na `ulegelege` wakufikiri na kutokujisumbua kusoma yalopita.
  Waandishi wa Habari tulikuwa na dhamana kubwa yakuufahamisha umma Mshindo Mkeyenge alikuwa ni nani? Alikuwa na mchango gani kwa Taifa na Tasnia ya Habari kwa Ujumla.
  Kama Yule Mwananchi wa kawaida atabaki na alama za kuuliza Mkeyenge ni nani? Na wewe Mwandishi wa Habari ubaki na alama ya kuuliza Mkeyenge alikuwa ni nani? Ni kwanini uwe mwandishi?
  Kuna Mwandhi mmoja `Mkongwe` wakati namweleza juu ya kifo cha Mshindo Mkeyenge akaniliuza Mkeyenge ni nani? Alinikatisha tama yakwenda kushiriki maziko yake lakini nilikwenda.
  Mwandishi alokuwa akiniuliza hivyo alianza kazi ya uandishi wa Habari mimi nikiwa shule ya Msingi.
   Inawezekana usikumbuke kila kitu kibinadamu lakani kama Mwandishi kwa mtu kama huyo lazima kengele italia aaahh..huyu nilimskia wapo huyu! Au huyu nilimsoma wapi huyu!! Tena mwandishi mwenyewe ni habari za Michezo ambaye Marehemu alibobea katikaUtangazaji wa Michezo na uongozi wa Timu ya Yanga.
  Ni sawa kwasasa waandishi wengi wa Habari ni vijana wa umri wangu,lakini hatujisumbui kusoma historia ya Nchi yetu na watu wake.
  Watu kama akina Tido Mhando,Ahmed Kipozi,ni baadhi ya watu waliyofanya kazi na Marehemu au ambao wanaweza kumuelezea kiufasaha Marehemu lakini ni Waandishi wangapi walikwenda kuwauliza juu ya Marehemu?
  Na walikuwepo Msibani na nilijaribu kuwauliza mawili matatu juu ya marehemu na walinijuza si machacche bali ni Mengi.
  Kuna baadhi ya waandishi ukiwauliza ni kwanini umechagua kuwa mwandishi wa Habari atakujibu ni kwasababu ya kuvutiwa na aina ya utangazaji wa mtu Fulani.
  Sasa hawa waandishi wa sasaivi walivutiwa na nani? Mbona hawajiangaishi kutafuta historia ya watu wa kabla yao? Tena watu wenye unasaba na taaluma zao!
  Kutokuwepo kwa waandishi wa Habari katika msiba wa Mkeyenge ni dhahiri hawaoni umuhimu wa vyombo vya vyao vya Habari kuwa na habari za Mkeyenge ambao hawamjui!!
  Hata hao wahariri hawaoni umuhimu? Unapokuwa Mwandishi wa Habari unapaswa kuwa mfuatiliaji wa mambo ya msingi yanayokuja na yalopita.
  Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo TASWA kimejaa watu makini nawaomba muendelee kutupiga msasa waandishi hasa wa habari za Michezo wanaokuja na hata hao wanaojiita wabobezi.
  Ingawa tabia ya mtu Ndiyo huakisi zaidi uandishi wake wa habari hivyo hata hizo semina hazitombadilisha ila itazidi kuwapa Mwanga wale wenye uandishi uliyopo ndani ya Damu.
  Kadhalika msanii Mkongwe Catherine John (62) maarufu Bi Nyakomba alifarikia Dunia ,Nilifika katika Msiba huo. Siwalazimisha Waandishi wa Habari kufika lakini Uzito wa Msanii huyo ni Habari katika Chombo chochote cha Habari na Taaluma inaelekeza Habari ni nini.
  Inawezekana hata chombo cha Habari kina Mhariri kijana asiyesoma ya Nyuma lakini kwanini hata msiulize?
  Bi Nyakomba mmoja kati waigizaji wa mwanzo katika Kituo cha Radio wakati huo Radio ni Moja tu ndiyo mmoja kati ya waasisi wa Michezo hii ya Kuigiza.
  Labda inaweza kutokea kwa vyombo vichache vikaelezea kwa makala maisha yake na mpaka mauti lakini siyo kwa wingi unaotakiwa kutokana na uelewa mdogo wa baadhi ya waandishi wa habari.
  Hawa wasanii wa kizazi hiki ambao wengi wao `hukaa uchi` majukwaani ndiyo vinara wakufuatwa na waandishi wa Habari na kuulizwa historia zao,na kupambwa katika kurasa kubwa zenye picha zao na sura zao na Bandia kuanzia rangi,kucha,Nywele,kope na hata maongezi ya kimagharibi.
  Ni ujinga mwingine unaoendekezwa na baadhi ya waandishi wa Habari. Sikatai waandikwe kama ni Habari lakini uandishi wa kivivu kushindwa kuujuza umma akina Mshindo Mkeyenge na Bi Nyakomba walikuwa watu gani ni uandishi unaochimbia kaburi tamaduni zetu.
  Msanii kama Bi Nyakomba angeitisha mkutano na Waandishi wa Habri kabla hajafa naamini wangefika waandishi wa Habari wachache sana. lakini aitishe mkutano Msanii mwenye `tabia mbovu `kama huyo Shilole, naamini waandishi wangekosa pakukaa. Kisa nini??
  Ndugu zangu waandishi wa Habari najua wengi wenu niwa miaka ya 1990 kuja mbele, lakini tuwa na utamaduni wa kusoma historia na kuwajua watu mbalimbali waliyovuma kwa tasnia mbalimbali.

  (Mwandishi wa makala haya ni mtangazaji wa Redio One na ITV, anayepatikanankwa namna +255 752 250 157 na +255 655 250 157)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BURIANI MSHINDO MKEYENGE, BI NYAKOMBA, LAKINI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top