• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 25, 2015

  SANGA WA YANGA ATEULIWA KUWA MAKAMU MWENYEKITI KAMATI YA MASHINDANO YA TFF

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemrejesha Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano.
  Uamuzi huo, umefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF jana- na Sanga atakuwa chini ya Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa wapinzani, Simba SC.
  Sanga anachukua nafasi ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati huyo, Ahmed ‘Msafiri’ Mgoyi.
  Clement Sanga (kushoto) amerejeshewa wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Mashindano ya TFF

  Wajumbe wa Kamati hiyo ni James Mhagama, Stewart Masima, Steven Njowoka na Said Mohamed- hii ikiwa Kamati iliyoteuliwa mara ya pili, (Februari 2015) tangu kupatikana kwa uongozi mpya wa TFF, chini ya Rais, Jamal Malinzi Oktoba mwaka juzi.
  Kamati ya kwanza kabisa ya Mashindano baada ya Malinzi kuingia madarakani, ilikuwa; Geofrey Nyange (Mwenyekiti), Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti) na Wajumbe Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed ‘Magari’, Gerald ‘Jerry’ Yambi, Davis Mosha, Said George na Nassor ‘Father’ Idrissa. 
  Lakini kutoka na baadhi ya Wajumbe kutokuwa wanahudhuria vikao, TFF ilifanya marakebisho Februari mwaka huu. 
  Inaaminika kurejeshwa kwa Sanga kunatokana na malalamiko ya Yanga SC, kwamba Kamati hiyo imekaa ‘Kisimba- Simba’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SANGA WA YANGA ATEULIWA KUWA MAKAMU MWENYEKITI KAMATI YA MASHINDANO YA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top