• HABARI MPYA

  Alhamisi, Mei 21, 2015

  SWAZILAND YAIBUTUA LESOTHO 2-0 COSAFA, SASA KUKUTANA NA MADAGASCAR KATIKA MECHI YA KIFO IJUMAA

  Na Mahmoud Zubeiry, RUSTERNBURG
  SWAZILAND imeendeleza wimbi la ushindi katika Kombe la COSAFA baada ya kuichapa mabao 2-0 Lesotho katika mchezo wa Kundi B usiku huu Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace mjini hapa.
  Swaziland sasa inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili sawa na Madagascar- maana yake timu hizo zitakutana katika mchezo mkali wa mwisho Ijumaa kuwania tiketi ya kwenda Robo Fainali.

  Mabao ya Swazi iliyoilaza 1-0 Tanzania katika mchezo wa kwanza Jumatatu, usiku huu yamefungwa na Xolani Sibandze dakika ya 43 na Tony Tsabedze dakika ya 66.
  Katika mchezo uliotangulia,Tanzania iliaga mashindano baada ya kufungwa manao 2-0 na Madagascar Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace pia.
  Huo unakuwa mchezo wa pili mfululizo timu hiyo kufungwa, baada ya awali kulala 1-0 mbele ya Swaziland Jumatatu na sasa itakamilisha ratiba Ijumaa kwa kumenyana na Lesotho kabla ya kurejea nyumbani.
  Mabao ya Madagascar yalifungwa na Rakotoharimalala Martin Njiva na Randriamanjaka Rinho Michel kipindi cha kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SWAZILAND YAIBUTUA LESOTHO 2-0 COSAFA, SASA KUKUTANA NA MADAGASCAR KATIKA MECHI YA KIFO IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top