• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 24, 2015

  NOOIJ APEWA NAFASI YA MWISHO TAIFA STARS, MUKEBEZI AREJESHEWA UMENEJA WA TIMU

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imempa nafasi moja ya mwisho kocha wa timu ya taifa, Mholanzi Mart Nooij juu ya mwenendo mbaya wa timu hiyo.
  Kamati hiyo iliyokuwa na kikao lao Dar es Salaam chini ya Rais wake, Jamal Malinzi imewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya COSAFA.
  Baada ya majadiliano ya kina, Kamati iliamua kumpa Mart Nooij changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee na 
  asipofanikisha hilo, mkataba wake utasitishwa mara moja.
  Mart Nooij sasa atalazimika kuiwezesha Taifa Stars kufuzu CHAN, vinginevyo safari imeiva

  Maamuzi haya yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi.
  Aidha, katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopold ‘Tasso’ Mukebezi amerejeshwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.
  Mukebezi alikuwa Meneja wa Taifa Stars tangu mwaka 2006 hadi mwaka jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NOOIJ APEWA NAFASI YA MWISHO TAIFA STARS, MUKEBEZI AREJESHEWA UMENEJA WA TIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top