• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 24, 2015

  RONALDO AMALIZA NA MABAO 61 LA LIGA REAL MADRID IKIPIGA MTU SABA

  MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefunga mabao matatu katika ushindi wa Real Madrid wa 7-3 usiku wa jana dhidi ya Getafe katika mchezo wa mwisho wa La Liga Uwanja wa Bernabeu.
  Hat-trick hiyo inamfanya Ronaldo afikishe mabao 61 msimu huu, ambao Real inamaliza bila taji, ikishika nafasi ya pili La Liga nyuma ya mahasimu, Barcelona na kutolewa na Juventus katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa.
  Mshambuliaji wa mkopo kutoka Manchester United, Javier Hernandez alifunga bao lake la kuagia Real ambalo lilikuwa la kwanza.
  James Rodriguez akafunga bao la tano wakati kinda Mnorway wa miaka 16, Martin Odegaard alitokea benchi kucheza mechi yake ya kwanza.
  Jese Rodriguez na beki wa kushito Mbrazil, Marcelo kila mmoja akafunga bao moja.
  Kocha Carlo Ancelotti anatarajiwa kuondoka Real na Rafa Benitez atachukua nafasi yake, lakini baada ya mchezo, Ronaldo akaposti kwenye Twitter: “Kocha babu kubwa wa namna yake. Natumai tutafanya kazi pamoja msimu ujao,” maana yake akimkingia kifua Ancelotti.
  The Portuguese forward netted three times, from open play, a free-kick and a penalty in the first period but Getafe clung on to go in at 3-3
  Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real mabao matatu katika ushindi wa 7-3 dhidi ya Getafe jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AMALIZA NA MABAO 61 LA LIGA REAL MADRID IKIPIGA MTU SABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top