• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 30, 2015

  NAMIBIA MABINGWA COSAFA 2015,, MADAGASCAR WATOA MFUNGAJI BORA

  TIMU ya taifa ya Namibia imetwaa Kombe la COSAFA mwaka 2015 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Msumbiji usiku huu Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
  Winga mwenye kasi, Deon Hotto ndiye aliyeibuka shujaa baada ya kufunga mabao yote dakika za 38 na 74, Namibia ikitwaa taji lake la kwanza kabisa la michuano ya nchi za kusini mwa Afrika.
  Na haikuwa kazi nyepesi kwao, kwani walianzia hatua ya makundi, wakiongoza Kundi A na kucheza jumla ya mechi sita ndani ya siku 14 hadi kubeba taji hilo.
  Katika mchezo uliotangulia, Madagascar ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Botswana mabao 2-1 kwenye Uwanja huo huo.
  Sarivahy Vombola alifunga mabao yote mawili kipindi cha kwanza dakika za 16 na 18 na kuibuka mfungaji Bora wa Kombe la COSAFA 2015 kwa jumla ya mabao yake matano, akiwazidi moja moja nyota wawili wa Namibia, Hotto na Benson Shilongo.
  Bao la kufutia machozi la Botswana limefungwa na Segolame Boy dakika ya 84.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAMIBIA MABINGWA COSAFA 2015,, MADAGASCAR WATOA MFUNGAJI BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top