• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 19, 2015

  RAHEEM STERLING AWA MWANASOKA BORA CHIPUKIZI WA MWAKA

  MSHAMBULIAJI Raheem Sterling amepata mapokezi mazuri katika usiku wa tuzo za Liverpool usiku huu ukumbi Echo Arena wakati anatajwa Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa klabu hiyo.
  Saa kadhaa baada ya kuelezwa amemuambia kocha Brendan Rodgers anataka kuondoka Anfield, kinda huyo wa umri wa miaka 20 aling'ara tena akipokea tuzo yake katikati ya Jiji. 
  Wakati anatoa hotuba fupi ya kushukuru kelele za 'Baki Raheem' zilitawala ukumbini, lakini alipomaliza na kuondoka walisikika baadhi ya watu kati ya mashabiki 3,000 wakizomea. 
  Raheem Sterling was named as Liverpool's young player of the year at their awards ceremony at the Echo Arena on Tuesday
  Raheem Sterling ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka Liverpool usiku huu ukumbi wa Echo Arena PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Wakati alipotajwa katika video iliyokuwapo ukumbini hapo kwamba anakwenda kuchukua tuzo, wengi walimshangilia.
  Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 alipanda basi moja na wachezaji wenzake wote jioni ya leo kutoka makao makuu ya Liverpool, Melwood kwenda ukumbi wa Echo Arena kwenye sherehe hizo. 
  Sterling alionekana akiwasili viwanja vya mazoezi na Range Rover yake nyeupe mchana kabla ya kupanda basi la wachezaji wakiwa wamevalia suti nyeusi nadhifu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAHEEM STERLING AWA MWANASOKA BORA CHIPUKIZI WA MWAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top