BAO la utata la Mfaransa Bafetimbi Gomis limeipa Swansea City ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Emirates, London.
Bafetimbi alifunga bao la dakika za lala salama kwa msaada wa teknolojia kwenye mstari wa lango, hicho kikiwa kipigo cha pili mfululizo kwa The Gunners.
Arsenal inabaki nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa pointi zake 70 ilizovuna katika mechi 35, ikiwa nyuma ya Manchester City wenye pointi 73 za mechi 36 na mabingwa, Chelsea wenye pointi 84 za mechi 36 pia.
Manchester United ni ya nne kwa pointi zake 68 za mechi 36 wakati Liverpool yenye pointi 62 za mechi 36 ni ya tano na Tottenham Hotspur yenye pointi 58 za mechi 36 ni ya sita.
Swansea wanaopanda nafasi ya nane sasa kwa kufikisha pointi 56 baada ya mechi 36, wanazidiwa pointi moja tu na Southampton walio nafasi ya saba.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin/Wilshere dk60, Cazorla, Ramsey, Ozil, Sanchez na Giroud/Walcott.
Swansea; Fabianski, Rangel/Richards dk60, Fernandez, Williams, Taylor, Cork, Dyer/Barrow, Shelvey, Ki/Gomis, Montero na Sigurdsson.
Befetimbi Gomis akishangilia baada ya bao lake la utata kukubaliwa na refa Kevin Friend PICHA ZAIDI GONGA HAPA


.png)
0 comments:
Post a Comment