• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 26, 2015

  MICHEZO YA MAJESHI YAANZA KUTIMUA VUMBI SONGEA


  Vikosi mbali mbali ya Majeshi vikiwa vimejipanga tayari kwa kungia uwanjani kwa ajili ya ufunguzi wa michezo ya majeshi 2015.

   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Songea Prof. Nomarn Sigalla King akisalimiana na wachezaji wa timu ya jeshi kutoka Mtwara.
  .........................................
  Na Amon Mtega ,SONGEA
  MICHEZO ya majeshi inayoshirikisha vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama briged ya kanda ya kusini imefunguliwa rasmi na kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Songea ,Pr Noman sigaa King huku benki ya NMB tawi la Songea likiwa limetoa msaada wa jezi za mpira wa miguu seti saba ambazo zenye thamani ya shilingi 3,000,000.
  Akiongea kwenye ufunguzi  huo  uliyofanyika leo katika uwanja wa michezo wa majimaji uliyopo Songea ,Sigara alisema kuwa  michezo hiyo itaimarisha mahusiano ya kiulinzi baina ya mipaka yetu ya Tanzania kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama vitakuwa na ushirikiano.
  Alisema kuwa ulinzi wa Tanzania katika mipaka yetu  hautegemei jeshi moja tuu bali ni ushirikiano wa vikosi vya majeshi mbalimbali kama vikosi hivi ambavyo vimeshirikishwa kwenye michezo hii iliyozinduliwa na ambayo itarajiwa kufanyika kwa wiki mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MICHEZO YA MAJESHI YAANZA KUTIMUA VUMBI SONGEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top