• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 27, 2015

  ARSENAL KUMKOSA DANNY WELBECK FAINALI KOMBE LA FA

  MSHAMBULIAJI Danny Welbeck ataukosa mchezo wa fainali ya Kombe la FA na pia hatakuwemo kwenye kikosi cha England kwa mechi za kirafiki za kimataifa mwezi ujao.
  Welbeck ameshindwa kupata ahueni tayari kwa mchezo na Aston Villa Jumamosi na pia atakosa mechi za England dhidi ya Jamhuri ya Ireland na Slovenia mwezi Juni.
  Kocha Arsene Wenger amesema: "Roy (Hodgson) alikuwa anajiamini kwamba atakuwapo, lakini tumewapigia simu FA jana kuwaambia kwamba goti lake halijapona na anahitaji kupumzika. Imekuwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa,". He scored a crucial winner against his former club Manchester United in the FA Cup semi-final at Old Trafford

  Danny Welbeck atakosekana Arsenal katika fainali ya Kombe la FA

  Welbeck hajacheza tangu aumie katika sare ya bila mabao na Chelsea Aprili 26 na Wenger amesema; "Hatakuwepo, nilijiandaa kwa hilo. Hajafanya mazoezi tangu Ijumaa iliyopita, hivyo nilijua atakosekana katika FA,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL KUMKOSA DANNY WELBECK FAINALI KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top