• HABARI MPYA

  Saturday, May 30, 2015

  KADO NA ‘MASTRAIKA’ WA UGANDA, KENYA WATUPIWA VIRAGO COASTAL

  Na Mwandishi Wetu, TANGA
  KIPA wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Shaaban Hassan Kado (pichani) aliyewahi kuwika klabu ya Yanga SC, ameachwa na klabu yake, Coastal Union ya Tanga.
  Uamuzi wa kumtupia virago kipa huyo wa zamani wa Moro United na Mtibwa Sugar za Morogoro umefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji cha Coastal Union kilichofanyika katikati ya wiki hii chini ya Kaimu Mwenyekiti, Steven Mguto.
  Akizungumza na Waandishi wa habari leo, Ofisa Habari wa Coasta Union, Oscar Assenga amesema kwamba kikao hicho kiliridhia kuwaacha wachezaji waliomaliza mikataba yao.
  Aliwataja wachezaji walioachwa mbali ya Kado wengine ni Keneth Masumbuko, Mganda Yayo Kato Lutimba, Suleiman Kibuta, Bakari, Razack Khalfan, Mkenya Itubu Imbem na Othman Tamim.
  Aidha, amesema kuwa wachezaji wengine ambao klabu imeamua kuwaacha ni Hussein Sued, Mansour Alawi, Amani Juma, Mohamed Mtindi na Mohamed Hassan.
  Hata hivyo, amesema wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao ambao klabu
  ipo kwenye mazungumzo nao kwa ajili ya msimu ujao ni Bakari Mtama, Rama Salim, Godfrey Wambura na Joseph Mahundi.
  Wakati huo huo, uongozi wa Coastal Union umewapandisha timu wachezaji wanne kutoka timu ya vijana kucheza timu ya wakubwa ambao ni Mtenje Albano, Tumaini Karim, Mohamed Twaha Shekue ‘Djong’ na Fikirini Suleiman ‘Mapara’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KADO NA ‘MASTRAIKA’ WA UGANDA, KENYA WATUPIWA VIRAGO COASTAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top