• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 26, 2015

  CAF YAIPA TANZANIA UENYEJI FAINALI ZA U17

  Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou 
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) leo hii limeipa Tanzania uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.
  Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali hizi. 
  Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.
  TFF imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fennela Mukangara kwa mchango wao wakati wa kuomba uneyeji.
  TFF pia inaamini ushirikiano huo wa Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano haya mwaka 2019. Hii ni mara ya kwanza kihistoria Tanzania kuwa mwenyeji wa Fainali za za Mataifa ya Afrika. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CAF YAIPA TANZANIA UENYEJI FAINALI ZA U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top