• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 22, 2015

  ‘BEKI MPYA’ YANGA SC ANAANZA LEO STARS NA LESOTHO

  Na Mwandishi Wetu, RUSTERNBURG
  BEKI Mwinyi Hajji Mngwali (pichani kulia) anayewaniwa na Yanga SC, atacheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwenye  michuano ya Kombe la COSAFA.
  Taifa Stars inamenyana na Lesotho jioni ya leo katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Kombe la COSAFA Uwanja wa Royal Bafukeng Sports Palace mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
  Na Mwinyi Hajji Mngwali wa KMKM ya Zanzibar alikuwa benchi katika mechi zote, Taifa Stars ikilala 1-0 mbele ya Swaziland na 2-0 mbele ya Madagascar.
  Mchezaji mwingine ambaye amekuwa akisugua benchi katika michuano hiyo aliyepata nafasi ya kuanza leo ni kiungo Hassan Dilunga.
  Deo Munishi ‘Dida’ atadaka mechi ya tatu mfululizo leo, wakati Shomary Kapombe ataanza beki ya kuli, Mngwali anachukua nafasi ya Oscar Joshua kushoto na katikati wataendelea kucheza Salim Mbonde na Aggrey Morris.
  Kiungo wa ulinzi, Erasto Nyoni, mbele yake Mwinyi Kazimoto na Hassan Dilunga wakati Simon Msuva na John Bocco watakuwa wanashambulia pale mbele.  
  Huo utakuwa mchezo wa 16 kwa Mholanzi Nooij kuiongoza Stars tangu awasili mwishoni mwa Aprili mwaka jana kuchukua mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen ikifungwa sita, sare sita na kushinda tatu katika mechi za awali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ‘BEKI MPYA’ YANGA SC ANAANZA LEO STARS NA LESOTHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top