• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 30, 2015

  RIO FERDINAND ASTAAFU SOKA, ATOA SHUKRANI ZAKE ZA DHATI KWA SIR FERGUSON

  BEKI wa zamani wa Manchester United na England, Rio Ferdinand ametangaza kustaafu soka baada ya kutemwa na klabu ya Queens Park Rangers.
  Uamuzi wa Ferdinand kutungika daluga zake unakuja akiwa katika majonzi ya msiba wa mkewe aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwezi Mei.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, ambaye alitangaza uamuzi wake katika mahojiano ya moja kwa moja na BT Sport, hivi karibuni ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwashukuru waliomtakia kila la heri baada ya kifo cha mkewe, Rebecca aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani, ambaye wamezaa naye watoto watatu.
  Ferdinand poses with then Manchester United manager Sir Alex Ferguson upon signing for the club in 2002
  Rio Ferdinand wakati anasajiliwa Manchester United akiwa na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Sir Alex Ferguson mwaka 2002

  MATAJI YA FERDINAND NA MABAO 

  Ligi Kuu (6): 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13
  Kombe la FA (1): 2003–04
  Kombe la Ligi (3): 2005–06, 2008–09, 2009–10
  Ngao ya Jamii ya FA (6): 2003, 2007, 2008, 2010, 2011, 2013
  Ligi ya Mabingwa Ulaya (1): 2007–08
  UEFA Super Cup (1): 2009 UEFA Super Cup
  Klabu Bingwa ya Dunia (1): 2008
  1996-2000: West Ham - mechi 127 mabao 2
  1996-1997: Bournemouth (mkopo) - mechi 10 
  2000-2002: Leeds United - mechi 54, mabao 2
  2002-2014: Man United - mechi 312, mabao 7
  2014-15: Queens Park Rangers - mechi 11
  1997-2011: England - mechi 81 mabao 3 
  Ferdinand amemtukuza kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwamba ni 'mjuzi' wakati akitoa taarifa yake kustaafu na akazungumzia anavyojivunia kuiwakilisha nchi yake.
  Amesema; "Baada ya miaka 18 yak kuwa mchezaji wa kulipwa, sasa nafikiri ni wakati mwafaka kustaafu mchezo ninaupenda.
  "Kushinda mataji katika miaka zaidi ya 13 niliyokuwa Manchester United, kuliniruhusu kufanikisha kila nilichokuwa natamani katika soka. Kutoka kijana mdogo hadi leo, nimepata mengi. Hakuna amnacho kingewezekana, bila mjuzi mmoja, Sir Alex Ferguson.
  Pia ningependa kumshukuru na kumuenzi marehemu mke wangu, Rebecca na familia yangu, akiwemo mama yangu na baba, kwa kujitolea kwao kwa ajili yangu, malezi yao na ushauri wao katika maisha yangu,". 
  Ferdinand, ambaye alianza kucheza kikosi cha wakubwa cha West Ham Mei mwaka 1996, ameshinda mataji sita ya Ligi Kuu ya England wakati wake akiwa Manchester United.
  Manchester United ilitoa kitita cha Pauni Milioni 30 kumnunua Ferdinand Julai mwaka 2002 na kumfanya awe beki ghali katika historia ya soka ya Uingereza wakati akisajiliwa kutoka Leeds United.
  Awali alinunuliwa kwa dau la Pauni Milioni 18 na Leeds kutoka West Ham lakini akacheza misimu miwili Elland Road kabla ya kutimkia kwa Mashetani Wekundu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RIO FERDINAND ASTAAFU SOKA, ATOA SHUKRANI ZAKE ZA DHATI KWA SIR FERGUSON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top