• HABARI MPYA

  Alhamisi, Mei 28, 2015

  ZAMBIA, MALAWI ZATINGA FAINALI YA ‘MAKAPUKU’ COSAFA, BAFANA NA GHANA AIBU YAO WENYEWE!

  Mchezaji wa Zambia akienda chini baada yaa kukwatuliwa na beki wa Ghana
  TIMU za taifa za Zambia na Malawi zimetinga Fainali ya vibonde Kombe la COSAFA maarufu kama michuano ya Plate ambayo itafanyika Ijumaa baada ya kushinda mechi zao za Nusu Fainali jana Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
  Zambia imewafunga Ghana mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza jana kabla ya Malawi kuwang’oa wenyeji, Afrika Kusini kwa penalti 5-4  kufuatia sare ya 0-0.
  Mabao ya waliokuwa mabingwa watetezi wa COSAFA, Zambia yalifungwa na Bornwell Mwape, Aaron Katebe na Nathan Sinkala.
  Ghana watakutana na Bafana Bafana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.
  Michuano ya wababe ya COSAFA leo inaingia katika hatua ya Nusu Fainali, Namibia ikimenyana na Madagascar Uwanja wa Moruleng Saa 11:00 jioni na baadaye Saa 1:00 usiku Botswana watamenyana na Msumbiji.B15E1MN0512
  Wachezaji wa Malawi (kulia) na Afrika Kusini (kushoto) wakigombea mpira jana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZAMBIA, MALAWI ZATINGA FAINALI YA ‘MAKAPUKU’ COSAFA, BAFANA NA GHANA AIBU YAO WENYEWE! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top