• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 30, 2015

  ARSENAL RAHA TUPU, WAIFUMUA 4-0 VILLA NA KUBEBA TENA NDOO YA FA ENGLAND

  KLABU ya Arsenal imefanikiwa kutetea Kombe la FA baada ya kuichapa mabao 4-0 Aston Villa katika mchezo wa Fainali usiku huu Uwanja wa Wembley, London. 
  Mshambuliaji Theo Walcott aliifungia bao la kwanza Arsenal dakika tano kabla ya mapumziko na Alexis Sanchez akafunga la pili dakika tano baada ya kipindi cha pili.
  Beki Mjerumani, Per Mertesacker naye akaifungia bao la tatu timu ya Arsene Wenger dakika ya 61, kabla ya Olivier Giroud aliyetokea benchi kufunga la nne dakika ya 90. 
  Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Ramsey, Ozil/Wilshere dk76, Sanchez na Walcott/Giroud dk76.
  Aston Villa: Given, Hutton, Okore, Vlaar, Richardson/Bacuna dk67, Cleverley, Westwood/Sanchez dk70, Delph, N'Zogbia/Agbonlahor dk52, Benteke na Grealish.
  The Gunners striker jumps for joy in front of the disappointed Villa fans as Arsenal inch closer to another FA Cup final victory 
  Alexis Sanchez akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia The Gunners katika ushindi wa 4-0 Kombe la FA PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL RAHA TUPU, WAIFUMUA 4-0 VILLA NA KUBEBA TENA NDOO YA FA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top