• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 22, 2015

  FIGO AJITOA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS FIFA

  MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Ureno, Luis Figo ametangaza kujitoa kwenye mbio za Urais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu. 
  Rais wa Chama cha Soka Uholanzi, Van Praag naye mapema alijitoa na kutangaza kumuunga mkono Prince Ali bin Al Hussein, ambaye atapambana na Rais wa sasa, Sepp Blatter.
  Mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa Ureno amesema katika taarifa aliyotoa kwenye ukurasa wake Facebook kwamba; "Nimefanya uamuzi wangu, sitasimama katika huo unaoitwa uchaguzi huo wa FIFA. 
  Figo amesema kwamba alikubali kugombea Urais kwa FIFA inahitaji mabadiliko hayo haraka, lakini ameshuhudia mambo ambayo yanaweza kumtia aibu yeyote mmoja anataka anataka kuikomboa soka.
  Luis Figo announced his intention to stand for the FIFA presidency on Wednesday
  Luis Figo ametangaza kujitoa kuwania Urais wa FIFA 
  Figo won 127 international caps for his native Portugal and scored 32 goals
  Figo aliichezea timu yake ya taifa Ureno mechi 127 na kuifungia mabao 32 

  WASIFU WA LUIS FIGO

  Umri: Miaka 42 
  Klabu alizochezea:
  Sporting (1989–1995) - mechi 137, mabao 16
  Barcelona (1995–2000) - mechi 172, mabao 30
  Real Madrid (2000–2005) - mechi 164, mabao 38
  Inter (2005–2009)- mechi 105, mabao 9
  Mechi za kimataifa: 
  Mechi 127 Ureno, mabao 32
  Mataji na tuzo: 
  Barcelona - La Liga mawili, Copa del Reys mbili, Kombe la Washindi la UEFA moja, UEFA Super Cup moja,
  Real Madrid - La Liga mawili, Ligi ya Mabingwa moja, UEFA Super Cup moja
  Inter Milan - Serie A manne, Coppa Italia moja
  Tuzo binafsi: 
  Mwanasoka Bora wa Ureno kuanzia 1995 hadi 2000
  Ballon d'Or mwaka 2000
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FIGO AJITOA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top